Home Kitaifa DC KALAMBO AFANYA UZINDUZI WA ZOEZI LA CHANJO YA POLIO

DC KALAMBO AFANYA UZINDUZI WA ZOEZI LA CHANJO YA POLIO

Na Mwandishi Wetu, Kalambo.

Mkuu wa Wilaya ya Kalambo iliyoko Mkoani Rukwa, Mhe. Tano Mwera amewataka kuhakikisha Wazazi wanawapeleka watoto wao wote walio chini ya miaka Mitano kupata chanjo ya matone ya Polio katika zoezi la siku nne, lililoanza rasmi Leo Septemba Mosi,2022.

Mhe. Tano Mwera ametoa kauli hiyo mapema leo wakati wa kuzindua zoezi hilo la chanjo ya Polio katika Kijiji cha Kisungamire,Wilayani hapa ambapo amesema ndani ya siku nne wawe wamehakikisha watoto wote walio chini ya miaka mitano wanapata chanjo.

“Ndugu zangu wa Kisungamire na Kalambo, Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama yetu Samia Suluhu Hassan
anatupenda sana na ndo maana anataka kuhakikisha afya za watanzania wote wakiwemo Wanakisungamire pamoja Wanakalambo wote zinaimarika, ndo maana zimeletwa hizi chanjo.

..tuhakikishe tunapata hizi chanjo bila kuchelewa, tuna siku nne tu hizi chanjo ziwe zimetembea kuhakikisha watoto wanapata chanjo hii.

Aidha, mbali ya kuzindua na kuhamasisha zoezi hilo la chanjo hiyo, Mhe.Tano Mwera amehamasisha zoezi la Sensa ambapo wale ambao bado kuhakikisha wanafikiwa kama ilivyotangazwa na Serikali ikiwemo kupiga simu maalum katika zoezi linaendelea ikawemo la Watu na Makazi.

Mwisho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!