
Na Shomari Binda-Musoma
MKUU wa Wilaya ya Musoma Juma Chikoka kesho jumamosi septemba 28 ataongoza mbio za polepole” Jogging” ya kujenga afya kwa wananchi.
Mbio hizo ambazo zitawashirikisha pia vikundi vya jogging vya mjini Musoma zitaanzia viwanja vya posta kuanzia saa 12 asubuhi.
Akizungumza mara baada ya kufanya makabidhiano rasmi ya ofisi na aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Musoma Dk.Khalphan Haule ambaye kwa sasa anahudumu wilayani Rorya amesema afya kwa wananchi ni jambo la msingi.
Amesema mazoezi ni sehemu muhimu ya kutengeneza afya na kama kiongozi lazima aongoze watu wenye afya bora.
Chikoka amesema kila mwananchi anapaswa kushiriki mbio hizo kwa kuwa ni za polepole na zitakuwa rafiki kwa kila mmoja.
Mkuu huyo wa Wilaya amesema kwa mujibu wa wataalam wa afya magonjwa yasiyo ya kuambukiza kama kisuksli na shinikizo la damu mazoezi ni sehemu ya kinga.
” Nawaalika wana Musoma kushiriki mbio hizi tutakazo zianza kesho kwa lengo maalum la kuweka afya zetu vizuri.
” Zoezi hili litakuwa endelevu kwani wananchi wanapokuwa na afya njema wanaweza kushiriki shughuli za kiuchumi”ameeema Chikoka.