
📍29 DISEMBA, 2024 – KILOLO, IRINGA
Mwenyekiti wa UWT Taifa Ndg Mary Pius Chatanda (MCC) amepokea salamu za pongezi kutoka kwa wananchi wa Kilolo mkoani Iringa kwa kazi kubwa ya ujenzi wa miundombinu anayoifanya.
Wananchi wa Kilolo mkoani Iringa wamemuomba Chatanda kufikisha salamu za shukrani na pongezi kwa Rais Samia kwa kutatua adha ya usafiri waliyokuwa wakikumbana nayo kwa muda mrefu kufuatia ujenzi wa barabara ya Ipogolo kwenda Kilolo kwa kiwango cha lami.
Aidha, wananchi wa Wilaya ya Kilolo wameahidi kujiandikisha kwa wingi ili kupiga kura za kishindo kwa Rais Samia ifikapo 2025.

