Home Kitaifa BOPOA wataka Elimu kutolewa ziwani kuepusha ajali

BOPOA wataka Elimu kutolewa ziwani kuepusha ajali

Na Neema Kandoro,Mwanza

WAMILIKI wa Boti na Yadi (BOPOA) Kanda ya Ziwa imeomba mamlaka zinazohusika kutoa elimu kwa watumiaji wa maji kuepuka kuingilia njia za meli ili vyombo hivyo vipite vizuri kuepusha ajali zinazoweza kuzuilika.

Hayo yamebainishwa jana Jijini Mwanza na Katibu wa BOPOA katika Kanda ya Ziwa Anwar Said alipokuwa akizungumza na Mzawa juu ya uzingatiaji wa usalama kwa watu na mali zao wanapotumia ziwa.

Alisema wanaomba mamlaka husika kutoa elimu kwa watu wanapokuwa ziwani ili kuepukana na matatizo ya kugongwa kwa wavuvi wanapokuwa wakivua samaki kwenye njia za meli hizo.

Vilevile elimu hiyo izidishwe ili tuweze kulinda mazingira na ekolojia ya viumbe majini dhidi ya uharibifu unaoendelea kutokea ziwani ” alisema Said.

Said alisema sambamba na hilo vilevile kumekuwepo matatizo ya nyavu kunaswa kwenye njia zipitazo meli hizo kwenye ziwa na hivyo kuwasababishia hasara wavuvi wa samaki.

Aliomba vilevile mamlaka hizo kuweza kuchora upya njia majini kwani kwani zimekuwepo kwa muda mrefu hivyo kuanza kufifia kwa kutokuonekana vizuri hali hiyo kuweza kusababisha adha kwa manahodha wa meli.

Said aliiomba vilevile Shirika la Wakala wa Meli Tanzania (TASAC) na Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) kufanyia matengenezo ya mara kwa mara bandari za watu binafsi kutokana na kukumbwa na changamoto ya kuziba kwa huduma za usafiri karibu na maeneo hayo kutokana na magugu maji yanayoletwa na maji.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!