
Na Deborah Lemmubi-Dodoma.
MKURUGENZI Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa Prof Abel Makubi amebainisha kuwa katika kipindi cha Serikali ya awamu ya sita huku wakitumia falsafa ya 4R za Dkt Samia Hospitali imepanua huduma za kibingwa kutoka 14 hadi 20 na huduma za ubingwa wa juu kutoka 7 hadi 16.
Ambapo huduma za ubingwa wa juu ni pamoja na upandikizaji wa figo,upandikizaji uloto, upasuaji wa mishipa ya damu,upasuaji wa moyo kwa kufungua kifua,uvunjaji wa mawe kwenye mfumo wa mkojo kwa kutumia mawimbi, upandikizaji wa uume,upasuaji wa ubongo na mfumo wa fahamu, upasuaji wa uti wa mgongo,kubadilisha nyonga na magoti,uoasuaji matundu madogo,matibabu ya mfumo wa chakula, matibabu ya magonjwa ya figo,uchujaji damu,matibabu ya magonjwa ya Moyo, uchunguzi na matibabu ya kiradiolojia, Tiba ya Magonjwa ya Hormone na kisukari na huduma za upatikanaji Mimba.
Prof. Makubi ameyasema hayo leo Jijini Dodoma Machi 2025 wakati akizungumza na waandishi wa Habari akielezea mafanikio ya Hospitali hiyo ndani ya miaka minne na kuelekea Maadhimisho ya miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita.
“BMH ikishirikiana na Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) zimekuwa zikitoa na kupanua huduma za tiba za kibingwa na Ubingwa wa juu wa Tiba na upasuaji kwa Wananchi mbalimbali wapatao million 14 kutoka mikoa zaidi ya 7 ya Tanzania. Katika kipindi cha Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Hospitali ya BMH, ikitumia falsafa ya 4Rs (Reforms, Rebuilding, Reconciliation na Resilience,), imepanua huduma za kibingwa kutoka 14 hadi 20 na huduma za ubingwa wa juu kutoka 7 hadi 16”.
“Huduma hizo za ubingwa wa juu ni ; Upandikizaji figo (kidney transplant), upandikizaji uloto (Bone marrow transplant), upasuaji wa mishipa ya damu (cardiovascular surgery), upasuaji wa Moyo kwa kufungua kifua (cardiothoracic surgery), uvunjaji wa mawe kwenye mfumo wa mkojo kwa kutumia mawimbi (external shock wave and laser lithotripsy) na upandikizaji uume(penile implantation), upasuaji wa ubongo na mfumo wa fahamu (neuro and spine surgery), upasuaji wa uti wa mgongo (spine surgery), kubadilisha nyonga na magoti (hip and knee replacement), upasuaji wa matundu madogo (laparoscopic and endoscopic surgery), Matibabu ya mfumo wa chakula (gastroenterology), Matibabu ya magonjwa ya figo (Nephrology), uchujaji damu (Dialysis), Matibabu ya magonjwa ya Moyo (cardiology), uchunguzi na matibabu ya mishipa ya moyo kupitia maabara ya uchunguzi (catheterization laboratory), uchunguzi na matibabu ya kiradiolojia (interventional radiology),Tiba ya Magonjwa ya Hormone na kisukari(Endocrinology and Diabeteology) na Huduma za upandikizaji Mimba (IVF)”.
Aidha amesema BMH katika kipindi hiki cha miaka minne imefanya upasuaji wa moyo kwa kufungua kifua kwa wagonjwa 60 kati ya hao watoto nib38 na watu wazima ni 22 na kiasi cha fedha kilichotumika ni shilingi milioni 562 lakini kati ya hizo milioni 100 zilitoka mfuko maalum wa Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan.
“Ndugu waandishi wa Habari, Katika kipindi cha miaka minne BMH imefanya upasuaji wa moyo kwa kufungua kifua kwa wagonjwa 60 kati ya hao watoto 38 na watu wazima 22. Kiasi cha fedha kilichotumika ni shilingi milioni 562 kati ya hizo milioni 100 zilitoka mfuko maalum wa Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan”.
“Aidha, Watalalamu wetu wamefanya Uchunguzi wa Mishipa ya Moyo (Cardiac Catheterization) kwa wagonjwa 1173, Upandikizaji Betri wagonjwa 23, kuweka vizibua njia ya mishipa ya moyo (Stents) kwa wagonjwa 42“.
Pia ameinisha mafanikio mengine kuwa ni pamoja na Upasuaji wa Ubongo na mishipa ya fahamu ambapo katika mika minne jumla ya wagonjwa 1061 kati yao upasuaji wa ubongo ni 771 na upasuaji wa uti wa mgongo ni 290. Aidha, wagonjwa 440 wamebadilishiwa nyonga na magoti.
Mbali na hayo ameelezea mwelekeo wao ambapo amesema wataboresha huduma ikiwemo matumizi ya akili unde,kuimarisha mifumo ya Tehama,kuanzisha huduma za matibabu ya mfumo wa fahamu bila upasuaji na Kitengo cha Kiharusi na matibabu ya Watoto wachanga.
“Ndugu waandishi wa Habari tumejipanga Kupandisha hadhi Hospitali kufikia Kiwango cha Hospitali ya Taifa Kuimarisha Mifumo ya TEHAMA katika kuboresha huduma ikiwepo matumizi ya AI katika huduma za kusaidia Wauguzi, customer care , robotic surgeries, upasuaji wa matundu Kukamilisha Miradi ya Mkakati ya Mindombinu inayoendelea Kujenga vituo vya umahiri vya Upandikizaji Figo (Japan), Uloto (EAC), Upasuaji wa Moyo, Upasuaji Ubongo, ENT , Mama na Mtoto na Tiba ya Macho Ujenzi wa Hostel ya Wagonjwa na Wageni Hospitali imekusudia kuanzisha huduma za matibabu ya mfumo wa fahamu bila upasuaji na Kitengo cha Kiharusi (Neurology and Stroke Unit), Matibabu ya magonjwa ya watoto wachanga (Neonatology), Rheumatology, Matibabu ya Mfumo wa Hewa (Pulmonology), Matibabu ya upasuaji wa marekebisho (Plastic Surgery), Matibabu ya Wazee (Geriatric Medicine)Kuendelea kusomesha na kuajiri Watumishi zaidi Kununua Vifaa vya Uchunguzi -Flowcystometry , Cachine za Radiotherapy and Nuclear machine, CT, MRI, Gene studies and therapy. Hitimisho Katika kipindi cha kuelekea miaka minne chini ya uongozi wa Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imewekeza kiasi cha shilingi bilioni 36.950 Kwaajili(dpf) na kuleta mafanikio malubwa katika huduma za kibingwa na Ubingwa bobezi”.
Hospitali hii ya Benjamin Mkapa, ilizinduliwa rasmi tarehe 13/10/2015, hivyo mwaka huu itakuwa inatimiza miaka 10. Ikiwa na Majukumu ya Kutoa huduma za Tiba za Kibingwa na Ubingwa wa juu kwa kutumia teknolojia ya kisasa Kutoa mafunzo ya Tiba na kufanya Tafiti mbalimbali zenye kuboresha uchunguzi na Tiba za magonjwa.
