Na Magreth Mbinga
TANESCO yatoa taarifa ya kukamilika kwa mipango ya muda mfupi ambayo waliahidi hivo imewezesha kupunguza makali ya mgao wa umeme walianza na kugawa wastani wa MEGAWATT 350 hadi 300 katika wiki iliyopita ilipungua iligawa MEGAWATT 200 hadi 250 .
Hayo yamezungumzwa na Mkurugenzi Mtendaji Tanesco Mh Maharage Chande na kusema kuwa mpaka kufika siku ya leo wanaga MEGAWATT 100 mpaka 150 kutokana n hatua ambazo wamechukua kwa kipindi cha muda mfupi.
“Tuliwaambia kwamba kituo chetu Cha Bwawa la kidatu kulikuwa na matatizo makubwa ya mashine nipende kuwatarifu kuwa ile mashine imerudi katika ubora na mashine zote zinafanya kazi”amesema Chande.

Pia Chande amesema mitambo ya muda mfupi wameitekeleza na wamebakisha mtambo mmoja wa MEGAWATT 20 wa Ubungo namba 3 ambao nao kabla mwisho wa Disemba utakuwa umekamilika na kuleta afueni kubwa.
“Katika kikao kile tulizungumza mipango ya muda wa kati tuliangalia kituo cha Kinyerezi namba moja cha upanuzi ambacho kitazalisha MEGAWATT 90 ambazo zitaingia kwenye gridi na tunajitahidi kufika februari tuweze kupata hizo nyingine ambazo tuliahidi ili kuendelea kupunguza changamoto tuliyonayo”amesema Chande.
Aidha Chande amesema kwa kutekeleza mipango ya muda mfupi wanaona mipango ya muda wa kati watafanikiwa sababu wanaimalizia na upungufu unaendelea kupungua na hivyo makali kuweza kupungua.
“








