

Na Boniface Gideon, TANGA
Wataalamu na wadau wa Afya wamekutana Jijini Tanga kwa ajili ya kutathmini
programu ya Wadau wa utoaji wa Elimu ya Afya kwa umma na ushirikiano
wa jamii kwa magonjwa ya milipuko wamesema kuwa serikali haitakubali
kusikia mlipuko wa ugonjwa wa ebola unaingia nchini.
Akizungumza katika ufunguzi wa kikao hicho, Mratibu wa Mafunzo ya Wahudumu wa Afya katika Wizara ya Afya, John Yuda
alisema kuwa wataalamu tiba hivi sasa wako kwenye mchakato wa ufuailia
kwa karibu chanjo ya ugonjwa huo wa ebola ambao umeripotiwa kulipuka
katika nchi jirani ya Uganda ili kujiridhisha na usalama wake kabla ya
kuruhusu matumizi yake kwa jamii.

“Tanzania sio kisiwa ambacho kinaishi kivyake. Hata chanjo ya za Uviko
zilikuwa nyingi na wataalamu walifanya utafiti mpaka walipojua kuwa ni
salama. Nasisi tunaendnelea na utafiti hado hapo tutakapojhiridhuisha
kuona kwamba kuna haja ya kuwa na chanjo au tujiridhsihe kuwa chanjo
hiyo ni salama na ndipo tutafanya maamuzi wakati huo. Kwa hiyo
tunasubiri,” alisema Yuda.
Hata hivyo alitoa rai kwa wananchi kuendelea kufuata ushauri wa
kitaalamu katika kuzuia. Tusingependa kusikia mlipuko unaingia
Tanzania,” alisisitiza na kueleza ushauri huo kuwa ni pamoja na jamii
kuzingatia kunawa mikono na iwe kama ni tabia au pale penye mkusanyiko
wa watu wajikinge kwa kuvaa barakoa kwa sababu hata ugunjwa wa Uviko
bado upo.
Kwa jamii ya mipakani alitoa rai kwa jamii kutoa taarifa mara moja
pale watapoona kuna mtu anayetoka katika maeneo ambaye yameripotiwa
kuwa na mlipukoili watalaamau wafuatilia kwa karibu na kuchukua hatua
zinazofaa.
Alisema ni muhimu kutoa taarifa kwa sababu jamii hizo za mipakani
zinashirikiana kwa karibu.
Mkutano huo unahudhuriwa na washirika wa maendeleo wa Tanzania
wanaofanya katika mikoa hiyo 11 na mashirika yanayofadhiliwa na
washirika hao. Washika hao ni pamoja na Shirika la kimataifa la Watoto
(UNICEF) ambao limefadhilia mkutano huo, Shirika la Afay Duniani
(WHO), CDC, USAID, Jihn Hopkins, BBC Media Action, Meducal Intrnation
na Help Age.
Mikoa hiyo ni Geita, Kagera, Kigoma,Mwanza, Mara, Arusha, Kilimanjaro,
Dar, Mbeya na Songwe na Ruvuma
Akifungua mkutano huo ambao umehudhruiwa pia na wajumbe wa kamati za
kitaalamu za mikoa na iwlaya kutoka mikoa 11 ambayo iko katika hatari
kutokana na kuwa na muingiliano wa watu kutoka katika nchi jirani
ikiwa ni mikoa yakanda ya ziwa, mikoa ya kusini na kusini magharibi ya
Tanzania na mkoa wa Dar es Salaam, Mratibu wa Tafiti na Machapisho
katika Wizara ya Twala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),
Kengia James alisema uwepo wa magonjwa ya milipuko katika nchi jirani
unatoa fursa ya Tanzania kujipanga kuzuia milipouko hiyo isije
Tanzania.
Pia alisisitizxa juu ya umuhimu wa kuwatumia viongozi wa dini katika
kutoa elimu, akieleza kuwa viongozi wa dini walitoa mchango mkubwa saa
katika kuhimiza watu kuchanja dhidi ya ugonjwa wa Uviko
James alisema kuwa katika kuimarisha kamati za utoaji wa elimu na
ushirikiano serikali imejairi maofisa afya 100 ambapo wamesambaza
kufanya kazi katika kamati hizo katika sehemu mbalimbali.


Naye Chipole Chipelembe, kutoka idara ya Afya na Ustawi wa Jamii,
TAMISEMI kitatumiwa na wataalamu na wajumbe wa kamati za utoaji Elimu
na Ushirikiano wa jamii watabadilishana uzoefu juu ya kazi walizofanya
na kujadiliana na kupata ufumbuzi wa changamoto mbalimbali ambazo
wamekutana nazo wakati wa utekelezaji wa kazi zao.
Alisema kuwa miaka mitatu iliyopita wakati ugonjwa Uviko ulipoingia
mifumo ya afya duniani kote iliingia katika mkanganyiko na sio
Tanzania pekee.
Alisema malengo ya kiako nijinsi mifumo ilivyopokea tatizo hilo,
kujiuliza kama raslimali zilitosha au walitekelezaje afua kuzuia
ugonjwa huo. Pia alisema wataiuliza kama wana takwimu za kutosha na ni
namna gani wanatumia takwimu hizo zilizokusanywa katika tafiti
“Kuna mikoa ambayo ilifanya vizuri na hivyo katika kikapo hicho
watabadilishan uzoefu na kutengeneza maazimio juu ya namna
watakavyokailiana na maginjwa hayo ya milipuko,” alisema.
Aliendelea kusema kuwa mkutano huo utaanagalia masuala ya uwajibikaji
na jinsi ya kuunganisha nguvu Alisisitiza juu ya umuhimu wa
ushirikiano wa jamii katika kutoa elimu kwa jami kuzuia milipuko
hiyo.
Mwisho