Home Kitaifa MATHAYO: HAKUNA MZAZI ANAYELIPA ADA YA MWANAFUNZI JIMBO LA MUSOMA MJINI

MATHAYO: HAKUNA MZAZI ANAYELIPA ADA YA MWANAFUNZI JIMBO LA MUSOMA MJINI

MBUNGE wa jimbo la Musoma mjini, Vedastus Mathayo amesema hakuna mzazi anayelipa ada ya mwanafunzi kwenye jimbo hilo.

Akizungumza kwa njia ya simu na Mzawa Blog kutoka bungeni Dodoma amesema ameshangazwa na taarifa kuwa wananchi wa jimbo la Musoma mjini wanalipa ada.

Amesema huo ni upotoshaji ulio wazi na wananchi wanapaswa kuzipuuza kwa kuwa wanafunzi wanaendelea kupata elimu pasipo vikwazo vyovyote.

Mathayo amesema serikali ya awamu ya 6 chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan,imeendelea kutoa fedha nyingi kwenye sekta ya elimu jimbo la Musoma mjini na hata michango ya ujenzi haipo.

Mbunge Mathayo amesema ni uzushi kudai wazazi wanalipa ada kwenye akaunti za shule na taarifa hizo hazina nia njema.

Nimemsikia Mwenyekiti wa (CHADEMA) Wilaya ya Musoma mjini akizungumza kwenye mkutano wa hadhara kwamba wazazi wanalipishwa ada jimbo la Musoma mjini huo ni uzushi mkubwa

“Wananchi wanapaswa kuzipuuza kwa kuwa wanafunzi wanaendelea kupata elimu pasipo vikwazo vyovyote vikiwemo vya ada”,amesema Mathayo.

Amesema amewasiliana na ofisi ya elimu msingi na sekondari halmashauri ya manispaa ya Musoma juu ya suala hilo na kuelezwa kuwa halipo.

Katika mkutano wa hadhara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) uliofanyika hivi karibuni mjini Musoma,Mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya Musoma mjini,Medard Shija,alidai wazazi kulipishwa ada shuleni.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!