Home Kitaifa Washauriwa kutumia Masoko ya Madini ya Mikoa kununua Madini Ili kuepuka vishoka.

Washauriwa kutumia Masoko ya Madini ya Mikoa kununua Madini Ili kuepuka vishoka.

Na Neema Kandoro Mwanza

Ofisa Madini Mkoani Mwanza Adrian Anthony ameyataka mataifa yenye kuhitaji kupata huduma hiyo kufika kwenye ofisi Masoko ya Madini yanayopatikana Mikoa yote nchini kwa ajili ya hitaji hilo na kuepuka watu wa mitaani wanaowafamyia udanganyifu.

Hayo yamebainishwa Jana kwenye kilele Cha Maonesho ya Biashara Afrika Mashariki Ili kuepuka udanganyifu unaoweza kufanywa kwao na watu wasio na nia njema.

Alisema serikali ilishaagiza mikoa yote hapa nchini kuwa na Masoko ya kufanyia biashara ya Madini ikiwa ni pamoja na katika Jiji la Mwanza ambapo ipo ofisi ambayo inasimamia Soko la Biashara ya itawauzia Madini ili watu wote wa ndani na nje ya nchi madini wanapata huduma hiyo.

Anthony aliwataka watu wote kutumia fursa ya uwepo wa maonesho hayo kununua madini toka kwenye taasisi yao ambayo inavyo vifaa vyenye Ubora wa kuhakiki na kupata ubora wa madini na kuepuka kununua mitaani ambapo wanaweza kuuziwa Vitu ambavyo si halali.

Kauli Mbiu ya Maonesho ya 18 ya Biashara Afrika Mashariki ni Mazingira bora ya biashara ni kitovu Cha kukuza Uwekezaji wa biashara Viwanda na kilimo Afrika Mashariki.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!