Shirika la viwango Tanzania(TBS)limewataka wafanyabiashara nchini kujiepusha na uzalishaji,uingizaji pamoja na usambazaji wa bidhaa zisizo na ubora ili kuepusha Tanzania kuwa dampo la bidhaa zisizo na ubora.

Akizungumza Jijini mwanza katika maonesho ya 18 ya biashara ya afrika mashariki,Meneja wa TBS kanda ya ziwa HAPPY KANYEKA amewahimiza wafanyabiashara kuzingatia sheria zilizopo ili kuepuka kupata hasara pamoja na kuchangia uharibifu wa mazingira.
Katika maonesho hayo yanayofanyika kwenye uwanja wa furahisha Jijini mwanza,shirika hilo limeibuka mshindi wa tatu miongoni mwa taasisi za umma nchini zinazojihusisha na masuala ya udhibiti.
Kauli mbiu ya maonesho hayo yanayozishirikisha zaidi ya makampuni mia tatu kutoka ndani na nje ya nchi ni MAZINGIRA BORA YA BIASHARA NI KIVUTIO CHA KUKUZA UWEKEZAJI WA BIASHARA,VIWANDA NA KILIMO TANZANIA,AFRIKA MASHARIKI NA AFRIKA KWA UJUMLA









