Home Kitaifa MBUNGE GHATI AZINDUA UJENZI NYUMBA YA KATIBU WA UWT WILAYA YA MUSOMA...

MBUNGE GHATI AZINDUA UJENZI NYUMBA YA KATIBU WA UWT WILAYA YA MUSOMA MJINI

Na Shomari Binda-Musoma

MBUNGE wa viti maalum mkoa wa Mara,Ghati Chomete, amezindua ujenzi wa nyumba ya Katibu wa UWT wilaya ya Musoma mjini.

Akiwa eneo la ujenzi huo mara baada ya kufanya uzinduzi amewashukuru viongozi ambao wameanza kuchangia katika hatua ya msingi.

Amesema katibu wa UWT wilaya ya Musoma mjini anafanya kazi kubwa ya kusimamia jumuiya hivyo anapaswa kuwa na makazi mazuri ambayo hayana usumbufu.

Ghati amesema kwa kuwa viongozi wameanza kuchangia na yeye anayo nafasi ya kufanya hivyo kuhakikisha nyumba hiyo inasimama.

Mbunge huyo amesema amepewa heshima kubwa ya kufanya uzinduzi wa ujenzi wa nyumba ya Katibu na kwa kuanzia anachangia tofali elfu moja( 1000).

Akizungumza na wajumbe wa baraza la UWT wilaya ya Musoma mjini na kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Mwisenge amewataka wanawake kupendana na kuwa wamoja.

Amesema wanawake wa UWT wasikubali kugombanishwa na.kuwataka kufanya kazi kwa pamoja kila mmoja kwenye eneo lake.

“Mmenipa heshima kubwa na mnaendelea kuniheshimisha na nyie kina mama.ndio mmenifanya kuitwa mheshimiwa”

“Kwa kuanzia kila Kata baada ya kupewa mafunzo ya ujasiliamali kwa kuanzia nawapa laki moja moja na sufulia kubwa 6 kwaajili ya kikundi cha UWT na viongozi wote nawapa vitenge kama zawadi na huu ni mwanzo” amesema Ghati.

Kwa upande viongozi hao wa Kata wa UWT wamemshukuru mbunge huyo kwa kuwapa mafunzo ya ujasiliamali na zawadi alizowapatia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!