Home Kitaifa MTANDAO MAJI YA BOMBA KUTOKA ZIWA VICTORIA YAENDELEA KUSAMBAZWA MUSOMA VIJIJINI

MTANDAO MAJI YA BOMBA KUTOKA ZIWA VICTORIA YAENDELEA KUSAMBAZWA MUSOMA VIJIJINI

Na Shomari Binda-Musoma

JIMBO la Musoma Vijijini lenye Kata 21, Vijiji 68 na Vitongoji 374. Vijiji vyote vina miradi ya maji ambayo iko kwenye hatua mbalimbali za utekelezaji kwa kasi kubwa.

Mbunge wa jimbo la Musoma vijijini, Profesa Sospetet Muhongo akiambatana na Kamati ya Siasa ya CCM ya Wilaya ya Musoma Vijijini kukagua miradi miwili ya maji ya bomba inayotekelezwa na Ruwasa amepongeza kasi ya utekelezaji.

Akiwa vijiji viwili vya Kata ya Bwasi vitakavyonufaika na upatikanaji wa maji ya bomba ya mradi wa Bwasi, Bugunda na Kome yenye chanzo cha maji kwenye Kitongoji cha Bujaga, Kijiji cha Bujaga, Kata ya Bulinga. Vijiji vitatu vya Kata ya Bulinga (Bujaga, Bulinga na Busungu) tayari vinapata maji ya bomba.

Muhongo amesema ujenzi wa tenki la ujazo wa lita 150,000 unakamilishwa na lipo kwenye Kitongoji cha Rugongo, Kijijini Bwasi bomba kuu la kusambaza maji limetandazwa kilomita 18 kati ya 31.5 na vituo vya kuchotea maji 25 kati ya 35 vimeishajengwa

Mradi huo una gharama ya shilingi milioni 997,714,196 ulianza februari 2023, utakamilishwa kabla ya oktoba 30 mwaka huu.

Kwa upande wa mradi wa Chumwi-Mabuimerafuru amesema unaanzwa kutekelezwa kwenye Vijiji vya Chumwi (Kata ya Nyamrandirira) na Mabuimerafuru (Kata ya Musanja) baadae utapanuliwa na maji yatasambazwa kwenye vijiji vingine vya Kata hizo mbili.

Chanzo cha maji ya mradi huu kiko ziwa victoria kwenye Kitongoji cha Nyachumwi Kijiji cha Chumwi

Amesema ujenzi wa tenki la ujazo wa lita 300,000 unakamilishwa kijijini cha Mabuimerafuru

Bomba kuu la kusambaza maji limetandazwa umbali wa kilomita 13 kati ya 24 na vituo vyote 17 vya kuchotea maji tayari vimejengwa huku gharama ya mradi ni shilingi bilioni 1.6.

Katika ziara hiyo wanavijiji walipata muda wa kutosha wa kuwasilisha kero na matatizo yao na majibu yalitolewa na mbunge wa Prof. Sospeter Muhongo. maswali yaliyohusu chama yalijibiwa na Mwenyekiti Ndg Denis Ekwabi na Katibu, Valentine Maganga

Wananchi wa jimbo la Musoma vijijini na viongozi wao wa ngazi zote wanaishukuru serikali chini ya uongozi mzuri wa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha za utekelezaji wa miradi yetu ya maendeleo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!