Na Shomari Binda-Musoma
WANAMICHEZO mkoani Mara,wameandaa bonanza maalum agost 8 siku ya nane nane kumkaribisha mkuu wa mkoa wa Mara,Saidi Mtanda.
Akizungumza na Mzawa Blog,mratibu wa bonanza hilo, Malvin Otieno amesema maandslizi yanakwenda vizuri kufanikisha bonanza hilo.
Amesema jumla ya timu 6 zitashiriki bonanza hilo la soka litakalotanguliwa na mbio za polepole”jogging” kuanzia saa 12 asubuhi.
Melvin amezitaja timu zitakazoshiriki bonanza hilo kuwa ni Biashara United veteran,Musoma veteran,Butiama veteran, Tarime veteran, 27 KJ Makoko veteran na Mara veteran.
Amesema timu zote zipo tayari kushiriki bonanza hilo ambalo litaganyika kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Karume mjini Musoma.
“Maandalizi yetu yanakwenda vizuri na timu zipo tayari kushiriki ili kumpokea mkuu wetu wa mkoa rasmi kama wanamichezo mwenzetu”
“RC Mtanda ni mwanamichezo na sisi kama wanamichezo tumeona tumpokee kwa kupitia bonanza hili la nane nane“,amesema Melvin.
Mratibu huyo amewakaribisha wananchi wote kushiriki bonanza hilo kuanzia saa 12 asubuhi ili kuweka mwili vizuri kiafya.








