Home Kitaifa TUIAMINI SERIKALI MAKUBALIANO YAKE NA SERIKALI YA DUBAI MKATABA WA DP WORLD

TUIAMINI SERIKALI MAKUBALIANO YAKE NA SERIKALI YA DUBAI MKATABA WA DP WORLD

Na Shomari Binda-Musoma

ASKOFU mkuu wa Kanisa la New Life Gospel Community Church (NLGCC) “Bonde la Baraka” Daniel Ouma,amewaomba wananchi kuiamini serikali kwenye mkataba uwekezaji wa bandari.

Kauli hiyo ameitoa kwenye mahubiri aliyoyatoa kwenye Kanisa hilo wakati wa ibada ya jumapili.

Amesema mijadala imekuwa mingi juu ya jambo hilo lakini serikali haiwezi kuwa na nia mbaya kwa wananchi wake zaidi ya manufaa.

Askofu huyo maarufu kwa jina la ” Dao” amesema ili kupunguza sintofahamu zilizopo serikali inapaswa kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kutumia vyombp vya habari yakiwemo magazeti.

Amesema wanasiasa wamekuwa wakiongea na kutofautiana na sasa serikali inapaswa kusimama na kutoa ufafanuzi kwa wananchi.

Dao amesema Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan,ni mtu mwema hivyo anaamini hawezi kuingia mkataba wa kuliangamiza taifa.

“Mjadala umekuwa mkubwa kila sehemu nami kupitia mazabahu haya ya bonde la baraka nishauri kwa serikali jambo la kupitia”

“Naiamini serikali kwenye jambo hili la uwekezaji wa BP World kwenye bandari ya Dar es salaam kwa manufaa yatakayopatikana sasa elimu itolewe ya kutosha kwa wananchi” amesema

Askofu Dao amesema wapo wanaosema nchi imeuzwa jambo smbalo halina afya nakuiomba serikali kusimama na kupinga kauli hizo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!