Home Kitaifa TANZANIA NCHI MWENYEJI WA MKUTANO WA RASLIMALI WATU UTAKAOHUDHURIWA NA MARAIS WOTE...

TANZANIA NCHI MWENYEJI WA MKUTANO WA RASLIMALI WATU UTAKAOHUDHURIWA NA MARAIS WOTE BARA LA AFRIKA

Na Magrethy Katengu

Tanzania ni mwenyeji wa Mkutano wa masuala ya raslimali watu wa Marais wa bara la Afrika na unaotarajiwa kuhudhuriwa na wageni wageni 1200 kutoka nchi zaidi ya 30 na kufanyika Julai 25-26 mwaka huu katika Ukumbi wa Kimataifa JNCC Dar es salaam .

Akizungumza na Waandishi wa habari Jijinj Dar es salaam Mkuu wa Mkoa Albert Chalamila amesema wananchi wa Mkoa wa Dar es salaam ndiyo mwenyeji wa Ugeni huo hivyo wananchi hawana budi kutumia fursa ikiwemo mahoteli,kupika vyakula vya kitanzani kwani hiyo ni sehemu ya utalii kujitangaza kupitia vitu vyao hivyo fursa zisiwaache nyuma itawasaidia kukuza kipato na kuimarisha uchumi

Mkutano huo unaofadhiliwa na Benki ya Dunia unatarajia kufanyika kuanzia Julai 25 hadi 26, 2023 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.

Tutakuwa na wageni wasiopungua 1200, ambao watakula, watalala na kutembelea sehemu zetu za utalii ikiwemo fukwe za bahari hivyo tayari maandalizi ya kutosha yamefanyika ikiwemo ulinzi wa kutosha , kujenga miundombinu ya barabara, huduma ya kwanza utalii wa Tanzania utajulikana katika kila mgeni atakayehudhuria” amesema Chalamila

Chalamila amesema Wageni wa mkutano huo wanatarajiwa kuanza kuwasili Dar es Salaam kesho Jumamosi Julai 22 na zaidi ya hoteli 40 zitatumika na wageni hao, hivyo mkutano huo pia ni fursa ya kutangaza utalii wa nchi na wamejiandaa kutangaza bidhaa zilizopo nchini kupitia mabanda ya wafanyabiashara.

Hata hivyo amesema washiriki wafanyabiashara wameshafanyiwa utaratibu wa kuleta bidhaa zao na mabanda yao watakuwa zaidi ya 100 na wamekwisha andaliwa vizuri kuhusiana na bidhaa, aina ya bidhaa, ujumla pia kujali wateja ‘customer care’ na kujiunga na maandalizi haya hakuhitaji gharama zozote,” amesema Chalamila

Pia amesema Mkutano huo ni matunda ya juhudi za Rais Dk. Samia Suluhu Hassan katika kuifungua nchi na kuwa kiongozi wa kutangaza utalii wa nchi ikiwemo utalii wa mikutano hivyo fursa mbalimbali zinaendelea kufunguka nchini

Naye Mkurugenzi wa Ukumbi wa Kimataifa JNCC Ephraim Makuru amesema Tanzania sasa kupitia kumbi zake kubwa imeweza kuendesha na kuwa mwenyeji wa mikutano ya kimataifa hivyo kwa takwimu zilizofanywa na taasisi Duniani inaonyesha Tanzania miaka ya nyuma ilikuwa nchi ya 13 kuwa na mikutano mikubwa ya kitalii na sasa inashikilia nafasi ya 5 kwa mikutano ya utalii

Aidha kumbi zote za JNCC kwa ajili mikutano zimekamilika na kwa kuwa kila nchi inahitaji kupata taarifa kwa lugha zao vifaa vimekamilika ili kila mgeni atakapoondoka kurudi nchini kwao aondoke akiwa na furaha na neno Ahsante Tanzania atamani kurudi tena

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!