Home Kitaifa CCM MKOA WA MARA KUJENGA UKUMBI WA KISASA WA MIKUTANO KWA MILIONI...

CCM MKOA WA MARA KUJENGA UKUMBI WA KISASA WA MIKUTANO KWA MILIONI 654

Na Shomari Binda-Musoma

CHAMA cha Maprnduzi ( CCM) mkoa wa Mara kimeanza ujenzi wa ukumbi wa mikutano na sherehe mbalimbali utakao ghalimu kiasi cha shilingi milioni 654.

Katibu wa CCM mkoa wa Mara Langaeli Akyo ametoa taarifa fupi ya ujenzi wa ukumbi huo kwa wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM mkoa wa Mara walipotembelea eneo la ujenzi kabla ya kuanza kwa kikao cha halmashauri.

Amesena kukamilika kwa ujenzi wa ukumbi huo wa kisasa kutawezesha kufanyika kwa vikao na kukodiwa kwaajili ya sherehe mbalimbali.

Akyoo amesema kiasi hicho cha fedha kitapatikana kutokana na michango ya wanachama na wadau mbalimbali.

Katibu huyo amewaeleza wajumbe hao kuwa jiwe la msingi LA ujenzi huo litawekwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara,Abdaraman Kinana,ambaye pia in mlezi wachama hicho mkoa wa Mara.

“Hadi kufikia hapa ulipofikia ukumbi wetu wapo viongozi waliochangia lakini tutajadiliana kuona kila mmoja anachangiaje kukamilika kwa ukumbi huo”

“Naamini ujenzi huo utakamilika kwa muda muafaka kwa kuwa ujenzi unaoendelea kama mlivyouona hausimami” amesema katibu huyo.

Mwenyekiti wa kamati ya ujenzi huo Mwita Gachuma amesema maendeleo ya ujenzi huo yanakwenda vizuri tangu ulipoanza.

Baadhi ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM mkoa wa Mara walioshiriki kikao hicho wamesema wapo tayari kuchangia na kutaka kupata utaratibu wa utoaji ikiwemo vifaa ili waweze kuchangia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!