Home Kitaifa WAZIRI WA ZAMANI WA KILIMO NA MIFUGO HERMAN KIRIGINI AFARIKI DUNIA

WAZIRI WA ZAMANI WA KILIMO NA MIFUGO HERMAN KIRIGINI AFARIKI DUNIA

Na Shomari Binda-Musoma

ALIYEKUWA mbunge wa zamani wa jimbo la Musoma vijijini na Waziri wa Kilimo na Mifugo Herman Kirigini amefariki dunia.

Akizungumza na Mzawa kwa njia ya simu mtoto wa marehemu na kada wa Chama cha Mapinduzi Paul Kirigini amesema mzee Kirigini amefariki mei 23 kwenye hospital ya rufaa ya mkoa wa Mara.

Paul amesema amepokea kifo cha mzee Kirigini kwa masikitiko makubwa kwa kuwa bado walikuwa wakihitaji ushauri wake.

Amesema hayo ni mapenzi ya Mungu na kilichobaki ni kumuombea na kuhusu taratibu za mazishi zitatolewa na familia.

Paul amesema msiba wa mzee Kirigini upo nyumbani kwake Kata ya Kamnyonge manispaa ya Musoma na taratibu nyingine za mazishi zikiendelea.

Marehemu Herman Kirigini,alikuws mbunge wa jimbo la Musoma vijijini toka mwaka 1980 hadi mwaka 1985 na licha ya Waziri wa Kilimo na Mifugo amewahi pia kushika nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya CCM na serikali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!