Na Magrethy Katengu.
KAMPUNI ya uuzaji wa Vifaa vya Magari (DAR QUALITY MOTORS) imesema itahakikisha inasambaza bidhaa bidhaa za spea za Magari aina zote zenye Ubora zaidi na kuepukana na bidhaa feki sokoni ili kusaidia wanazotumia bidhaa zao wawe na uhakika wa vyombo vyao vya moto wawapo Barabarani.

Akizungumza Leo Jijini Dar es salaam Afisa Masoko wa Kampuni Shamsa Mselemu Wakati wakimkabidhi Ubalozi Shabiki wa Klabu ya Yanga Maarufu anayejulikana kwa jina la Mzee Mpili amesema wamemchagua Mzee huyo kutangaza bidhaa zao kutokana na Umaarufu wake katika mitandao mbalimbali ya kijamii
“Dunia inakwenda kasi Kimtandao hivyo lazima Wafanyabiashara na sisi tuwe na ubunifu wa hali ya juu kutumia mitandao ya Kijamii kujitangaza hivyo kupitia Mzee Mpili tuna Imani naye Kampuni yetu ya bidhaa za spea za Magari hiyo ikiwemo Mabasi,Malori ataitangaza ndani na nje ya mipaka ya Tanzania”amesema Shamsa.
Naye Balozi Mzee Mpili amesema amemshukuru sana Kampuni hiyo kwa kumuamini kuitangaza hiyo kampuni hivyo atahakikisha kupitia Umaarufu wake bidhaa itajulikana ndani na nje ya mipaka ya Tanzania
Aidha Mzee Mpili ni Shabiki wa Klabu ya Yanga Leo amekabidhiwa Ubalozi na Kampuni hiyo katika Ofisi ya Biashara iliyoko Tabata Dar es salaam hivyo wateja wote wanakaribishwa kununua bidhaa hizo kwa bei ya gharama nafuu na inasafirishwa hadi mikoani








