NA Magrethy Katengu
Imeelezwa kuwa mgonjwa mmoja wa Kifua kikuu akiwa hajaanza matibabu ana uwezo wa kuambukiza watu kati ya 10-20 kwa mwaka kwa hivyo ni vyema walio karibu nao kuchukua tahadhari mapema ili kusaidia kupunguza ugonjwa huo kuendelea kuenea kwa kasi
Mratibu wa Kifua Kikuu na Ukoma Jiji la Dar es salaam Dkt Mbarouk Seif amesema Mgonjwa ambaye hajapata matibabu ana uwezo wa kuambukiza watu hivyo ni vyema endapo kati ya Jamii anayoishi nayo wakigundua miongoni mwao ndugu,jamaa,Rafiki amekwenda kupima na kugundulika ana TB nao waende wakafanyiwe vipimo mapema kwani kuna huduma ya kinga au matibabu mapema kabla ugonjwa haujawa sugu”amesema Dkt Seif
Kifua Kikuu kinatibika na kupona kabisa na mgonjwa akianza tiba hawezi kuambukiza matubabu ya TB hutolewa chini ya utaratibu wa mgonjwa kusimamiwa kumeza dawa kila siku katika kituo cha kutolea huduma za afya au nyumbani
Hata hivyo Dkt Seif amesema wakati mwingine anayetakiwa kumsimamia ni Msimamizi nyumbani anaweza kuwa mume,Mke,ndugu,ndugu,mwanafamulia au mtoa huduma ngazi ya Jamii hivyo hao wanaokuwa karibu na mgonjwa kama Kinga zao za mwili siyo Imara kuzuia dhidi ya magonjwa yanayobukizwa Kwa njia ya hewa ni budi nao kufanya vipimo
Dkt Seif amesema ugonjwa wa kifua Kikuu huweza kujitokeza katika mwili kama uvimbe na huweza kukaa shingoni,mgongoni hivyo Daktari anayechukua vipimo itambidi kukata sehemu ya kinyama kwenye uvimbe na kufanya vipimo na akigundua kuwa ni kifua Kikuugonjwa hupewa dozi aanze Ili aweze kupona .
Naye Mmoja wa Mkazi aishie Wilaya ya Kilombero Mkoa wa Morogoro Kata ya Mang’ula Anna Msovela kwa njia ya simu akizungumza na Mwandishi wetu kwa njia ya simu amesema namna TB ilivyomuua mumewe na yeye akaugua lakini alipona amesema ukweli yeye ni miongoni mwa wahanga aliugua Kifua kikuu kwa kuambukizwa na Mumewe marehemu wakati akimuuguza mnamo Mwaka 2014 .
Bibi Msovela amesema Mumewe alikuwa anatumia kilevi na Uvutaji Sigara hivyo kutokana na Matumizi vitu hivyo alianza kukohoa taratibu baadaye akaanza kutoa makohozi meusi hivyo wakaanza kutumia dawa za kienyeji kufikiria amelogwa na hali ilizidi kuwa mbaya akaanza kutoa makohozi yaliyochanganyika na damu homa joto kali kukosa hamu ya kula ndipo wakaenda tena Mkoani Iringa kumfanyia Matambiko wakifikiria amekosea mizimu lakini bila mafanikio yeyote.
Bibi Msovela anaendelea kuelezea kuwa hali ilivyozidi kuwa mbaya wakabidi wampeleke katika kituo cha Afya Mang’ula akapewa rufaa aende hospitali ya Ifakara baada ya kufanyiwa vipimo alibainika kuwa Mumewe anaugua Kifua kikuu huku akiambiwa Mapafu yake yakionyesha yametoboka hivyo akalazwa Mwezi mzima na akapewa Dozi za kutumia
“Mume wangu nilimsimamia atumie dawa vizuri alivyoruhusiwa kutoka kituo cha afya baada ya kupata nafuu na kurudi nyumbani lakini baada ya miezi saba nafuu ilianza kuonekana akaanza kula vizuri kukohoa damu kuliisha akaingia tamaa tena ya kurudia kutumia Uvutaji wa sigara kwa Siri huku akiwa anatumia dawa siku Moja alitoroka na kunyws Pombe kupiliza wakati alizuiwa na alirudi akiwa amelewa na usiku huo huo hali yake ya afya ilibadilika akakimbizwa kituo cha afya na kifo kilimkuta tukarudisha mwili wake nyumbani tukamzika“amesema Bibi Masovela
Bibi .Msovela amesema kwa kukiri kuwa TB inawezekana mtu kupona endapo mgonjwa atazingatia masharti na utaratibu aliopewa na daktari ikiwa kama alizuiwa ila kuacha mazoea mabaya ya matumizi ya Uvutaji sigara,bangi,kujidunga na akikaidi maelekezo na kuacha dawa kabla ya wakati kifo chake ni uzembe wake mwenye japo nilimpenda mume wangu na kufanya jitihada ziliishia patupu.
Bibi Msvela ameendelea kusimulia hata hivyo baada ya kufariki Mumewe kwa Kifua kikuu alikaa miezi 9naye akaanza kukohoa mara kwa mara hivyo alivyoenda hospitali alifanyiwa uchunguzi na kugundulika ana kifua kikuu ndiyo kinaanza alianza dozi kwa muda wa miezi kadhaa akapona kabisa na hakufikia hali mbaya kama aliyofikia Mumewe.
“Naishukuru sana Serikali sana kwa kutusaidia kutupa huduma ya Kifua kikuu bure bila kuchangia chochote ila anaiomba kuhakikisha ikiwa mgonjwa aliyegundulika na kifua kikuu Muuguzaji wake wa karibu apewe kinga kama ni vidonge au sindano na jamaa yake wa karibu wafanyiwe vipimo wote ili kusaidia kupunguza idadi ya Wagonjwa”amesema Bibi Msovela

Naye Mratibu Kifua kikuu Mnazi Mmoja Dkt Linda Mutasa amesem Wahudumu wa afya wanakutana na changamoto ya wagonjwa ambao hawamalizi dozi na wanarudi wakiwa wanaumwa tena hali zao zikiwa mbaya hivyo hulazimika kuwasimamia wanywe dawa wakiwa wanawaona kutokana na baadhi yao wakipatiwa dawa wakianza kupata nafuu huacha dozi hivyo wanaporudi hospitali hutulazimu kutumia njia hiyo kusaidia janga hili la ugonjwa wa TB kupungua na maambikizi yake”amesema Dkt Lind








