Home Kitaifa DIWANI MANIFREDI LYOTO AMWONA RAIS SAMIA HASSAN MWANAMKE MWENYE UPEKEE WAKE

DIWANI MANIFREDI LYOTO AMWONA RAIS SAMIA HASSAN MWANAMKE MWENYE UPEKEE WAKE

Na Magrethy Katengu

Diwani wa Kata ya Mzimuni Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Manfred Lyoto amekiri kumpa Mwanamke kuwa daraja la kwanza kwani imejidhihirisha kwa mara ya kwanza Rais it. Samia Suluhu Hassan kuonesha mwenye kujali bila Ubaguzi Machi 8 2023 kuhudhuria Mkutano wa Wanawake wa Chadema uliofanyika Mkoani Kilimanjaro ni Ujasiri wa Kisiasa .

Akizungumza leo Jijini Dar es salaam chombo cha habari Mzawa blog amesema haijawahi kutokea tangu Taifa hili kupata uhuru miaka 30 iliyopita Rais kuhudhuria Mkutano wa Chama Pinzani kimoja kama Mgeni Rasmi na kuhutubia zaidi inaonekana tu viongozi wa vyama pinzani kuitwa Ikulu hivyo Rais huyo ameonesha unyenyekevu pekee sana katika uongozi wake kwani analiongoza Taifa na hapendi kuona chuki za Kisiasa inahitaji watu wenye Upendo Amani .

“Katiku maisha yangu Mimi Mwanamke nampa heshima kubwa sana kwani yeye huweka Mtoto tumboni mwake miezi 9 na ndiye mwamuzi wa kuamua afe au aishi hivyo tuangalie Nchi yetu imekuwa na Mfululizo wa Marais watano wanaume Mfululizo na katika hao alivyoingia Rais Samia Suluhu Hassani ametudhihirishi mwanamke ni mwenye huruma kujali utu,Upendo kama kukitokea jambo lolote anatuita mezani tunazungumza tunakubaliana kivitendo “amesema Diwani

Sanjari na hayo amesema Mwanamke kupewa Madaraka katika nchi yeyote inakuwa ya tofauti hebu iangaliwe Mfano Nchi ya Swiden wanaishi vizuri sana hivyo wasio na ufahamu huongea kuwa hawawezi ni uongo Miradi iliyoachwa na Hayati John Pombe Magufuli inaendelea na mingine ameuanzisha dharau na kejeli dhidi yake acheni

Diwani Lyoto izungumzia juu ya uyeusu utekelezaji uliofanywa katika kata ya Mzimuni chini ya Ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM amesema katima sekta ya elimu na afya ndiyi kipaumbele zaidi ambapo tayari baadhi ya changamoto amezipatia ufumbuzi japo siyo kwa asilimia miamoja.

Pia amefafanua katika Sekta ya Elimu amefanikwa kujenga uzio unaozunguka shule ya Sekondari Mzimuni, Shule ya Msingi Mzimuni na Mikumi ambapo ujenzi huo umekamilika na kuondoa adha kuingiliana na wananchi na kupunguza utoro kwa wanafunzi wanaosoma shuleni hapo.

Aidha Diwani Lyoto amesema kulikuwa na changamoto ya uhaba wa madarasa hivyo kupelekea wanafunzi wanaonza darasa la kwanza na kidato cha kwanza kuingia shuleni kwa awamu mbili hivyo serikali imejenga majengo ya kutosha na mwaka huu wameingia shuleni kwa awamu Moja na wote wanakaa kwenye madawati hadi madarasa yamebaki

“Waalimu walikuwa wanapata adha ya kutembea kwenda Kigogo kuchapisha mitihani hivyo Kwa fedha zangu mwenyewe nimegharamia kununua mashine ya kuchapishia mitihani(photocopy Machine) ambayo inauwezo mkubwa hivyo inatumiwa na shule zote tatu za Sekondari Mzimuni Shule ya Msingi Mzimuni “amesema Lyoto

Hata hivyo amesema Ili kusaidia kukuza taaluma ya mwanafunzi na kuondokana na sifuri alikaa na waalimu na wazazi kuangalia namna ya kuwaezesha wanafunzi kupata angalau mlo mmoja kwa siku hivyo wazazi walikubaliana kuchangia TSH 1000 kila siku kwa ajili ya chakula na yeye kama Diwani kununua kontena lenye gharama zake mwenyewe k ili kutumika kwa ajili ya kuhifadhia chakula na iwe kama ofisi ya kuratibu chakula kwa wanafunzi wa shule na kukarabati jiko akiununua vifaa vya jiko,ambapo tayari wanafunzi wameanza kupata chakula cha mchana shuleni hapo.

“Kiongozi lazima uwe unatumikia wanafunzi kwa kile Mungu alichokubariki kwani serikali inafanya Mambo mengi yenye na huwa inatenga bajeti lakini huwezi kusaidia kila mahali hivyo lazima wananchi tunapoona tunauwezo kuisaidia tujitoe kwani ni Kwa faida yetu sote na kizazi kijacho kujenga Taifa letu Bora” amesema Diwani

Akizungumzia kuhusu sekta ya afya amesema kulikuwa na changamoto ya Watumishi ikiwemo Madaktari Wauguzi kati zahanati ya Kata ya Mzimu ,lakini katika uongozi wake wa miaka miwili tangu 2022 alipochaguliwa kuwa diwani wa kata hiyo ameleta watumishi watatu ambao ni daktari mmoj,Muuguzi (nes)mmoja na Mtaalamu wa Maabara na amewajibika yeye mwenyewe Diwani kuwalipa mshahara kila mwezi kama hivyo kwasasa wananchi wanapata huduma kwa wakati tofauti na hapo awali watumishi waliku wawili tu na foleni kubwa ya wagonjwa.

Kuhusu Miundombinu ya barabara amesema kuwa tayari barabara ya kutoka Magomeni Mapipa hadi Mabibo imekamilika na Magomeni kuna Flyover hivyo Maendeleo yanakwenda kwa kasi ya haraka Achini ya Ilani ya Chama cha CCM ikisinamiwa na Mwanamke Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!