Home Kitaifa ELIMU NA MAFUNZO KWA WAZEE NI MUHIMU SANA KISARAWE -DC NYANGASA

ELIMU NA MAFUNZO KWA WAZEE NI MUHIMU SANA KISARAWE -DC NYANGASA

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mhe Fatma Almasi Nyangasa amezindua kituo cha jamii cha kujifunzia (Community Learning Center) Kata ya Mzenga kilichofadhiliwa na shirika lisilo la kiserikali la DVV international Feb 2023

Aidha ameshukuru DVV international kwa mchango wao katika kuhakikisha wazee wanapata fursa ya Elimu katika mazingira mazuri. Vilevile, Mh. Mkuu wa Wilaya amewataka wananchi wa Mzenga kukitunza Kituo na kukitumia kwa ajili ya kujishughulisha na shuguli za uzalishaji Mali na kujipatia kipato.

Kwa niaba ya Watu wa Kisarawe tunawashukuru Sana kwa Kupata Eneo Hili la Elimu ambavyo wazee wetu watapata mafunzo Pia mewataka waweke mfumo mzuri katika kufuatilia mafunzo hayo kwenye kusoma na katika uzalishaji mali kwa kufanya hivyo Kata ya mzenga haitokua na Watu Wazima wasiojua Kusoma lakini pia itawasaidia kufika malengo yao kiuchumi” alisisitiza Mhe Nyangasa

Uwepo wenu hapa inaonesha mnamatamanio ya kufanya vizuri hivyo mkawe wahamasishaji wazuri kwa wengine ambao hawajaona hii kama fursa nzuri” alisema Mhe Nyangasa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!