Na Magrethy Katengu
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe Mwanahamisi Mkunda amewaomba wale wote wanaoomba mikopo ya Halmashauri ya asilimia 10 iliyotengwa na serikali kuwanufaisha vijana,Wanawake,na watu wenye ulemavu kurejesha kwa wakati Ili na wengine wanufaike ambapo mpaka sasa waliorejesha wamefikia 60%

Ombi hilo amelitoa leo Jijini Dar es salaam wakati akifunga Mafunzo ya Ujasriamali, Usimamizi wa biashara na fedha kwa vikundi 183 vya wanawake Vijana na watu wenye ulemavu wanufaika na 10% ya mapato ya ndani 2022 ,2023 ambapo amesema fedha hizo zinazotolewa na Dkt Rais Samia Suluhu Hassani hutolewa kwa awamu.

”Tunafahamu mikopo ya Mabenki inavyoumiza kutokana na kurejesha kwa riba lakini mkopo wa asilimia kumi unaotolewa ya Halmashauri hutolewa pasipo kuwa na riba yeyote hivyo nasihi rejesheni kwa wakati ili kila mmoja apate” amesema Mkuu wa Wilaya.
Mwanahamisi amesema Dkt Rais Samia aliongeza bajeti ya utoaji mikopo isiyo na riba inasaidia wananchi kutatua changamoto zaidi ya moja kwenye jamii, Ili kusaidia kila mwananchi awe na uchumi imara ni Niya yake ya dhati taifa liwe lenye uchumi jumuishi.
“Tokea kuanza kwa utoaji mikopo hiyo kumechochea kuzalisha ajira mpya nyingi kwenye jamii hivyo wanavikundi waanzishe miradi mbalimbali inayokwenda kutatua changamoto za jamii,ikiwa ni pamoja na kufungua zahanati,Viwanda “ amesema Mkunda
Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Temeke Abdalah Mtinika amesema Wilaya hiyo inaoongoza Mkoa wa Dar es salaam kwa wananchi wake kurejesha fedha wanazokopeshwa ambapo mpaka Sasa wamefikia asilimia 60
Naye Mbunge wa Temeke Dorothy Kilave amesema Dkt Rais Samia Suluhu Hassani anawapenda sana Wananchi wake hivyo ametoa Bilioni 11 na milioni 18 Ili kutatua changamoto za kiuchumi kwa watu wake anaowaongoza
Afisa biashara manispaa ya temeke judith matage Amewakumbusha wajasiliamali na wafanyabiashara kukata leseni za biashara na kwamba ni takwa la kisheria kabla ya kufungua biashara unatakiwa ukate leseni kwanza na lazima zibandikwe ukutani.
“Ukiomba leseni ni masaa 24 tu,vikundi vyote mnatakiwa muwe na leseni,mahitaji yake ni lazima muwe na katiba,muhtasari,TIN,Mkataba wa pango,cheti cha usajili wa vikundi cha mwisho ni vitambulisho vyenu,vingine ni vya kibiashara niwakaribishe ofisini”

Kwa upande kikundi Cha Taifa kilichonufaika na Mkopo wa Halmashauri ya Temeke Mwakilishi wao Christopha Mjema amesema waliomba Mkopo mwaka 2019 mwaka 2020 walipewa kiasi cha fedha 40 wakaanzisha kampuni ya uuzaji pikipiki na Temeke na Gongolamboto na wamefanikiwa kuajiri vijana 9 hivyo na wamefanikiwa kufikisha milioni 68 mwaka huu mwezi wa 7 mwaka huu wanakamilisha kurejesha fedha zote
Naye Thomasi Richard ambaye aliyeomba Mkopo mwaka huu amesema wameomba Mkopo Kwa ajili ya kuwasaidia kufungua Zahanati katika Halmashauri hiyo kutoka na kuona kuwa eneo walilochagua wananchi wanatembea umbali mrefu kufuata huduma.








