Tume ya Tehema Tanzania (ICTC) leo tarehe 13 Februari 2023 Imesaini mkataba wa ushirikiano na UNESCO kwa ajili ya utafiti wa matumizi ya interneti.
Awali Mkurugenzi wa ya Tume ya TEHAMA Nkundwe Moses Mwasaga Alimshukuru Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa jitihada zake kubwa anazofanya za kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji katika uchumi wa kidigitali. Lakini pia aliwashukuru sana UNESCO kwa kuamua kushirikiana nao na kuwaahidi kuhakikisha utafiti unaenda kufanyika unaweza kusaidia katika utekelezaji wa sera za kitaifa katika mapinduzi ya TEHAMA.

Mkurugenzi wa Tume Ya TEHAMA Nkundwe Moses Mwasaga alisema utafiti huu kwa Tanzania ni wa kwanza na ulipaswa kufanyika kwa muda mrefu kwani matumizi ya interneti yameanza kitambo kidogo.
“Kiukweli utafiti kama huu kwa nchi yetu ulitakiwa kufanyika muda mrefu sana kwani masuala ya interneti haujaanza leo Tanzania”
Pia Nkundwe Moses Mwasaga amebainisha kuwa Tume ya TEHAMA ndio inasimamia sera ya taifa kwenye TEHAMA na utafiti huu utaisaidia Tume katika utekelezaji wa kazi zao.
“Tume ya TEHAMA ndio inasimamia sera ya letu kwenye TEHAMA hivyo utafiti huu ni muhimu sana kwani pia itatusaidia sisi kama tume katika utekelezaji wetu”
Lakini pia Mkurugenzi mtendaji wa UNESCO Tanzaniae Mr Michael Toto alisema ICTC na UNESCO zinasaini mkataba huo kwa ajili ya ushirikiano wa utafiti kuangalia maendeleo na matumizi ya intaneti Tanzania. na mkataba huu ni mwitikio wa wito wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ambapo mwaka jana Tarehe 14 Februari 2022 alipowasili Makao makuu ya UNESCO Paris Ufaransa aliwasihi kuendelea kutoa ushirikiano wa katika kujenga jamii yenye usawa nauelewa wa Masuala mbalimbali ya Teknolojia.

Utafiti huo utanazamiwa kukamilika ndani ya miezi mitatu na baada ya hapo matokeo ya utafiti yatatumika katika utekelezaji wa sera mbalimbali za Masuala ya teknolojia Nchini.
Pia Mr Michael Toto alisema UNESCO inatarajia utafiti huo utaenda kutoa majibu ya utekelezaji wa sera na kuboresha matumizi ya intaneti Tanzania na kuangalia Tanzania inavyoweza kunufaika na kuitangaza Lugha ya Kiswahili na kupatikana katika mifumo ya intaneti.

Mwisho Mkurugenzi wa Tume ya TEHAMA Nkundwe Moses Mwasaga aliwahikishia Wanachi kupitia waandishi wa habari kuwa utafiti ukikamilika wataita tena kuwaambia nini kinaendelea.

=================








