
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya mabadiliko ya muundo wa Wizara mbili kwa kuzitenganisha ili kuongeza ufanisi katika utendaji wa Serikali.
Wizara hizo ni Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, ambayo sasa imegawanywa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa pamoja na Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Aidha, Wizara ya Mifugo na Uvuvi imegawanywa na kuwa Wizara ya Mifugo na Wizara ya Uvuvi.













