Home Kitaifa Dodoma Kuwa Mwenyeji Wa Maadhimisho Ya Siku Ya Ukimwi Duniani 2026.

Dodoma Kuwa Mwenyeji Wa Maadhimisho Ya Siku Ya Ukimwi Duniani 2026.

Celebrating 25 Years of NHIF

Mkoa wa Dodoma unatarajia kuwa mwenyeji wa Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani mwaka 2026, yatakayofanyika Desemba 1, huku wananchi wakihamasishwa kujitokeza kwa wingi kupata elimu na huduma mbalimbali za afya zitakazotolewa katika kipindi cha maadhimisho hayo.

FAHARI AFYA

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma, Mkuu wa Mkoa Mhe Rosemary Senyamule amesema Maadhimisho hayo ni fursa muhimu ya kuwakumbuka watu waliopoteza maisha kutokana na UKIMWI, kuwaenzi wanaoishi na VVU na kutathmini mafanikio pamoja na changamoto zilizopo katika juhudi za kudhibiti Maambukizi ya VVU nchini na duniani kote.

Aidha Senyamule ameishukuru Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) kwa kuipa Dodoma nafasi ya kuwa mwenyeji wa maadhimisho hayo, huku akimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kuimarisha sekta ya afya kupitia ujenzi wa hospitali, vituo vya afya na zahanati, pamoja na upatikanaji wa dawa za kupunguza makali ya VVU (ARV) bila malipo.

Na kuongeza kuwa maadhimisho hayo yataanza kwa maonyesho ya wadau wa kudhibiti VVU na UKIMWI kuanzia Novemba 24 hadi Desemba 1, 2026, katika viwanja vya (JKCC), Dodoma na Katika kipindi hicho, wananchi watapata huduma za ushauri nasaha na upimaji wa hiari wa VVU, upimaji wa saratani ya shingo ya kizazi, sukari, pamoja na elimu ya kinga dhidi ya VVU na huduma nyingine za kijamii, ikiwemo huduma za NIDA, RITA na msaada wa kisheria.

Ambapo amesema kilele cha maadhimisho hayo kitafanyika Desemba 1, 2026, katika ukumbi wa JKCC, ambapo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi ambapo Maadhimisho hayo yataambatana na kumbukumbu ya miaka 25 tangu kuanzishwa kwa TACAIDS mwaka 2001.

Maadhimisho haya yanaongozwa na kauli mbiu inayosema “Huduma Bora za Afyani ni Msingi wa Kutokomeza Ukimwi“.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!