Home Kitaifa WATANZANIA WAHIMIZWA KUSHUHUDIA UZINDUZI MTUMBA

WATANZANIA WAHIMIZWA KUSHUHUDIA UZINDUZI MTUMBA

Celebrating 25 Years of NHIF

Na Deborah Lemmubi – Mzawa Media, Dodoma

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, kwa niaba ya Kamati ya Maandalizi, ameridhishwa na maandalizi ya uzinduzi wa majengo ya ofisi za wizara na taasisi za Serikali, pamoja na barabara za lami katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.

FAHARI AFYA

Prof. Mkumbo amebainisha hayo leo, Oktoba 29, 2026, baada ya kukagua maeneo mbalimbali yatakayotumika katika hafla hiyo, ikiwemo Uwanja wa Mashujaa.

Katika ziara hiyo, ameupongeza uongozi wa maandalizi kwa kazi iliyofanyika na kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kushuhudia tukio hilo la kihistoria.

Uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika kesho, Oktoba 30, 2026, ukihudhuriwa na Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na Rais wa Angola, João Manuel Gonçalves Lourenço.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!