
Na Deborah Lemmubi – Mzawa Media, Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, amesema kuwa Serikali imejenga Mji wa Serikali Mtumba, Dodoma, kwa kuzingatia kiwango kikubwa cha utoaji wa huduma, sambamba na kufanya uwekezaji mkubwa katika mifumo ya uendeshaji wa shughuli za Serikali.

Msigwa ameyasema hayo leo, Oktoba 28, 2026, katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma, baada ya ziara ya wahariri na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini, iliyofanyika leo kuelekea hafla ya uzinduzi wa majengo ya wizara na taasisi za Serikali pamoja na barabara za lami katika mji huo.
Amesema kuwa huduma zinazotolewa kwa sasa katika Mji wa Serikali Mtumba zinafanyika kwa ufanisi zaidi kupitia mifumo maalumu iliyowekwa kwa ajili ya kurahisisha utoaji wa huduma na uendeshaji wa Serikali kimtandao.










