Home Kitaifa TANZANIA KUNUFAIKA NA TAFITI NA UWEKEZAJI KATIKA SEKTA YA NISHATI

TANZANIA KUNUFAIKA NA TAFITI NA UWEKEZAJI KATIKA SEKTA YA NISHATI

Celebrating 25 Years of NHIF

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Luswetula, kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar, ameongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa 35 wa Bodi ya Magavana wa Taasisi ya Kujenga Uwezo Afrika (The African Capacity Building Foundation – ACBF) na Mkutano wa Afrika wa Taasisi za Tafiti na Majadiliano ya Sera (Africa Think Tank Summit – ATTS), utakaofanyika jijini Cotonou, Jamhuri ya Benin, tarehe 28 hadi 30 Oktoba 2026.

Mkutano huo utakaowakutanisha viongozi wa Serikali, watunga sera, watafiti, wataalamu, sekta binafsi na washirika wa maendeleo kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika, unalenga kujadili nafasi ya tafiti, uimarishaji wa uwezo wa taasisi na mageuzi ya sera katika kukabiliana na changamoto za maendeleo barani Afrika, hususan katika sekta ya nishati, uwekezaji, ukuaji wa uchumi na uboreshaji wa huduma kwa wananchi.

jose

Tanzania inatarajiwa kujumuika na wadau wengine kujadili upatikanaji na ugharamiaji wa nishati ya umeme kwa kuangalia namna sekta ya nishati inavyoweza kutumika kama kichocheo cha kuongeza uzalishaji, ushindani na ukuaji wa uchumi jumuishi.

Kupitia majadiliano yatakayofanyika, Tanzania inatarajiwa kupata fursa ya kubadilishana uzoefu na wadau mbalimbali kuhusu namna ya kuvutia uwekezaji katika miundombinu ya nishati, kuboresha mifumo ya usimamizi wa sekta ya umeme na kutumia teknolojia zinazoweza kuongeza ufanisi wa uzalishaji na usambazaji wa nishati ili kujenga sekta ya umeme iliyo imara na inayoweza kuchangia kikamilifu katika mageuzi ya kiuchumi barani Afrika.

Sambamba na masuala ya nishati, mikutano hiyo inalenga kuimarisha nafasi ya tafiti na ushahidi wa kitaalamu katika uandaaji na utekelezaji wa sera za maendeleo, ambapo Tanzania inatarajia kupata maarifa mapya, kuboresha upangaji wa mipango na kuimarisha uwezo wa taasisi katika kutekeleza vipaumbele vya Taifa vilivyoainishwa katika Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050 (Dira 2050).

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!