Home Kitaifa RC SENYAMULE ARIDHISHWA HALI YA UJENZI UWANJA MPYA WA MPIRA NZUGUNI JIJINI...

RC SENYAMULE ARIDHISHWA HALI YA UJENZI UWANJA MPYA WA MPIRA NZUGUNI JIJINI DODOMA.

Na Deborah Lemmubi-Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Rosemary Senyamule leo ametembelea mradi wa ujenzi wa Uwanja mpya wa Mpira unaojengwa katika eneo la Kata ya Nzuguni Jijini Dodoma,ambapo amesema amefurahishwa na hatua iliyofikiwa pamoja na utayari na utashi wa Wakandarasi katika kufanya kazi yao.

Ambapo ameahidi kama Mkoa kuendelea kutoa ushirikiano kwa changamoto yeyote ili kazi hiyo ya ujenzi iende kwa haraka na ubora uliokusudiwa.

RC Senyamule ameeleza hayo leo Agasti 11,2026 Jijini Dodoma katika Ziara yake alipotembea na kukagua hali na hatua za ujenzi wa Uwanja huo unajengwa katika eneo Nzuguni Dodoma.

“Vinginevyo tumefurahishwa na ziara hii, tumeendelea kufurahishwa na Wakandarasi ambao wameonesha utayari wa kufanya kazi yao kwa utashi mzuri, na sisi kama tuahidi kama Mkoa kukiwa na changamoto yeyote tuko hapa kwaajili ya kushirikiana ya kushirikiana ili kufanya kazi hii iende kwa haraka na ubora uliokusudiwa”.

Aidha ametumia nafasi hiyo kuwasihi wote waliopata dhamana ya kuwa sehemu ya kufanikisha mradi huo hasa vijana wahakikishe kuwa kazi yao kubwa inakuwa ni kulinda rasilimali za nchi ambazo zimewekezwa katika mradi huo.

Kwa kuhakikisha kuwa ubora uliokusudiwa unazingatiwa katika ujenzi huo ili uwanja uwe mzuri na wa viwango na kutoa taarifa pale wanapoona vitendo vya uharibifu pale vitu visipoenda sawa.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Serikali kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Edwin Godfrey amesema kuwa ujenzi wa uwanja huo kwasasa uko asilimia 14 na wako katika ujenzi wa wa jukwaa la kwanza ambapo uwanja utakuwa na uwezo wa kutabeba watazamaji 32,500.

Na kuongeza kuwa ajira zilizopo ni wa Watumishi 210 hadi 300 kwa wiki na kati yao wageni ni 20 hadi 30 na wanaosalia ni Wazawa na kusema uwanja huo una sifa ya daraja la nne ambalo daraja hilo kwa wasamizi wa Caf ni daraja la juu kwa kiwanja.

Naye Emmanuel Mang’ombe moja ya vijana na kiongozi katika mradi huo ameiomba Serikali kuendelea kuwekeza miradi mikubwa kama hiyo kwa wageni na wazawa ili vijana kuendelea kupata ajira nchini.

Upendo Charles naye amesema mradi huo umekuwa na manufaa ya moja kwa moja kwa vijana na wa Tanzania kwa ujumla kwani imetoa ajira kwa watu wa elimu ya ngazi ya juu hadi watu wa elimu ya ngazi ya chini ambapo huwapa nafasi ya kupata ujuzi inapotokea nafasi kama hii.

Ujenzi wa Uwanja huu wa mpira Katika eneo la Nzuguni Jijini Dodoma uko chini ya Makampuni Limonta na utagharimu zaidi ya Bilioni mia tatu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!