Mwenza wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Neema Mwigulu Nchemba, amehimiza Taasisi za umma na binafsi kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuboresha huduma za kijamii kupitia utekelezaji wa programu za uwajibikaji kwa jamii (CSR).
Ameyasema hayo, Juni 16, 2026 katika hafla ya kukabidhi vifaa vya hospitali vilivyotolewa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) katika Hospitali ya Wilaya ya Chamwino, Mkoa wa Dodoma, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Shirika hill.
Aisha, Mama Neema ameishukuru, Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji mkubwa katika sekta ya afya hususani katika ujenzi wa Hospitali, utoaji wa ajira kwa wataalamu wa atya, upatikanaji wa dawa na vifaa tiba pamoja na kuimarisha huduma za kibingwa na ubingwa bobezi ziliOrahisisha upatikanaji wa huduma bora za afya nchini.
Amesema vifaa hivyo vilivyotolewa vinajumuisha vitimwendo 20, vitanda vya kujifungulia vitano, vitanda vya kufanyia uchunguzi vitano, vitanda vitano vya kulaza wagonjwa, machela moja ya kisasa, makabati matatu ya kuhitadhia vitaa tiba pamoja na mabeseni yenye vifaa mbalimbali kwa ajili ya akinamama 30 waliojifungua vitasaidia vitasaidia kuboresha utoaji wa huduma katika Hospitali ya Wilaya ya Chamwino na kuongeza ustawi wa mama na mtoto.
Awali, akimkaribisha mgeni rasmi kuzungumza katika hafla hiyo, Waziri wa Viwanda na Blashara, Judith Kapinga amesema Serikali itaendelea kuhimiza taasisi zake kutekeleza kwa vitendo sera ya uwajibikaji kwa jamii ili kuchangia kuboresha huduma za kijamii na maisha ya wananchi.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule, amesema Mkoa wake uko tayari katika kushirikiana na Wizara Pamoja na TBS kwa ujumla katika kuendeleza Sekta ya Viwanda na Biashara na jitihada za uwajibikaji kwa Jamii katika Mkoa wake.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya (TBS) Profesa Othman Chande na Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt. Ashura Katunzi wamesema TBS itaendelea kutekeleza sera yake ya kuwajibika kwa jamii (CSR Policy) ili kuendelea kuwa karibu na jamii katika kuleta tija na maendeleo.



















