Home Kitaifa BONDIA MMAREKANI AFURAHIA MAPOKEZI TANZANIA, AJIANDAA KUONA MAAJABU YA SERENGETI

BONDIA MMAREKANI AFURAHIA MAPOKEZI TANZANIA, AJIANDAA KUONA MAAJABU YA SERENGETI

Bondia wa kimataifa wa Marekani Terence “Bud” Crawford amesifu ukarimu wa Watanzania tangu alipowasili nchini Mei 24, 2026, kwa ziara ya kitalii.

Bondia huyo ameyasema hayo alipokutana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi jijini Dar es Salaam akianza ziara yake ya siku kadhaa nchini.

Bondia huyo mwenye rekodi ya kutopoteza pambano lolote katika michezo 42 aliyocheza tangu aingie ndondi za kulipwa, ameeleza pia kusubiri kwa hamu kuona maajabu ya vivutio kama Serengeti, Ngorongoro na Zanzibar atakakotembelea.

Kwa upande wake Dkt. Abbasi kwa niaba ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), amemkaribisha nchini na kumwalika kuendelea kuja Tanzania kila atakapohitaji hasa wakati huu ambapo ameamua kustaafu mapema mchezo huo tangu Disemba mwaka jana 2025.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!