Home Kitaifa WAFANYABIASHARA WAOMBA KUBORESHEWA MAZINGIRA YA KUFANYIA BIASHARA

WAFANYABIASHARA WAOMBA KUBORESHEWA MAZINGIRA YA KUFANYIA BIASHARA

Wafanyabiashara wa nyanya na mbogamboga katika soko la Mirongo jijini Mwanza wameiomba serikali kuwaboreshea eneo lao la biashara ili kuwanusuru kuungua na jua na kunyeshewa mvua kutokana kuwa wazi, maboresho ya soko hilo yaliyofanywa miaka miwili iliyopita na shirika la kutetea haki za wanawake na Watoto la KIVULINI

Mkurugenzi wa shirika la kutetea haki za wanawake na Watoto KIVULINI Yassin Ally amesema ipo haja kwa halmashauri zote nchini kuhakikisha wanaweka mpango kazi wa kuboreshewa masoko katika halmashauri ili wajasiliamali wadogo waweze kufanya biashara katika mazingira yaliyo bora.

Mwenyekiti wa umoja wa wanawake wa Chama cha mapinduzi ( UWT ) Marry Chatanda amekabidhi mifuko ya saruji 55 kwa ajili ya kuboresha eneo la wafanyabishara wa nyanya na mbogamboga lililopo eneo la Mirongo jijini Mwanza ili kuhakikisha linakarabatiwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!