Na Shamimu Nyaki
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma, na Maendeleo ya Jamii inayoongozwa na Mwenyekiti Stanslaus Nyongo ambaye ni Mbunge wa Maswa Mashariki, imepokea taarifa ya Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ambapo imepongeza Wizara hiyo kwa kuendelea kufanya mageuzi katika wizara hiyo.

Pongezi hizo zimetolewa na Wajumbe wa Kamati hiyo wakati wakitoa maoni, ushauri na mapendekezo mbalimbali, baada ya kupokea Taarifa hiyo iliyowasiliswa na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Pauline Gekul, Januari 24, 2023 Dodoma.

Akizungumza baada ya kupokea taarifa hiyo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Nyongo amesema, wizara hiyo imeendelea kufanya maboresho mbalimbali ambayo yanasaidia wadau wake kujiajiri, kupata kipato na zaidi kuchangamsha nchi kupitia Sekta zake.









