
Mkazi wa Dar es Salaam, Jerome Mushi, amejishindia pikipiki aina ya TVS kupitia promosheni ya “Shinda Boda” inayoendeshwa na kampuni ya michezo ya kubahatisha ya PigaBet Tanzania.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa zawadi hiyo, Mushi alisema ushindi huo ni fursa muhimu kwake kwani anatarajia kuitumia pikipiki hiyo kuanzisha shughuli ya usafirishaji wa bodaboda ili kujiongezea kipato pamoja na kumpatia ajira kijana mwingine.

Alisema vijana wengi wanatafuta njia mbalimbali za kujikwamua kiuchumi, hivyo anaamini ushindi huo utamsaidia kuanza shughuli ya bodaboda na kuboresha maisha yake.
“Ushindi huu utanisaidia kuanza kazi ya bodaboda na pia kumpa nafasi kijana mwingine kupata ajira,” alisema Mushi.
Alieleza kuwa amekuwa akishiriki katika michezo hiyo kwa muda na mara kadhaa alipata ushindi mdogo mdogo kabla ya kupata ushindi huo mkubwa.
Kwa upande wake, Afisa Masoko wa PigaBet Tanzania, Hemed Msonge, alisema promosheni ya “Shinda Boda” imeanzishwa kwa lengo la kutoa fursa kwa washiriki kujishindia pikipiki.
Aliongeza kuwa katika promosheni hiyo pikipiki hutolewa kwa washindi wanaopatikana kupitia droo zinazofanyika kila wiki kwa kipindi cha kampeni hiyo.








