Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Wanu Hafidh Ameir, akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Afrika ya Chakula Shuleni na Siku ya Kimataifa ya Chakula Shuleni yaliyofanyika leo Machi 12, 2026, jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Wanu Hafidh Ameir, akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Afrika ya Chakula Shuleni na Siku ya Kimataifa ya Chakula Shuleni yaliyofanyika leo Machi 12, 2026, jijini Dodoma.


Sehemu ya wanafunzi wakimsikiliza Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Wanu Hafidh Ameir (hayupo pichani) wakati wa maadhimisho ya Siku ya Afrika ya Chakula Shuleni na Siku ya Kimataifa ya Chakula Shuleni yaliyofanyika leo Machi 12, 2026, jijini Dodoma.


Sehemu ya wanafunzi wakimsikiliza Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Wanu Hafidh Ameir (hayupo pichani) wakati wa maadhimisho ya Siku ya Afrika ya Chakula Shuleni na Siku ya Kimataifa ya Chakula Shuleni yaliyofanyika leo Machi 12, 2026, jijini Dodoma.



Sehemu ya washiriki wakifuatilia hotuba ya Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Wanu Hafidh Ameir (hayupo pichani) wakati wa maadhimisho ya Siku ya Afrika ya Chakula Shuleni na Siku ya Kimataifa ya Chakula Shuleni yaliyofanyika leo Machi 12, 2026, jijini Dodoma.


Wanafunzi wakisoma risala pamoja na kucheza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Afrika ya Chakula Shuleni na Siku ya Kimataifa ya Chakula Shuleni yaliyofanyika leo Machi 12, 2026, jijini Dodoma.



Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Wanu Hafidh Ameir akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzungumza katika maadhimisho ya Siku ya Afrika ya Chakula Shuleni na Siku ya Kimataifa ya Chakula Shuleni yaliyofanyika leo Machi 12, 2026, jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna-DODOMA
SERIKALI kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imeendelea kuwahimiza wadau wa elimu kuunga mkono mpango wa utoaji wa chakula mashuleni, hatua inayolenga kuboresha mahudhurio,ufaulu wa wanafunzi, afya pamoja na maendeleo ya wanafunzi shuleni.
Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Wanu Hafidh Ameir, wakati akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Afrika ya Chakula Shuleni na Siku ya Kimataifa ya Chakula Shuleni yaliyofanyika leo Machi 12, 2026, jijini Dodoma.
Mhe. Ameir amesema mpango wa chakula shuleni una mchango mkubwa katika kuboresha afya na uwezo wa wanafunzi kujifunza, kwani watoto hutumia muda mwingi wakiwa shuleni kuliko nyumbani.
Amesema upatikanaji wa chakula bora, maji safi na mazingira salama ya usafi ni muhimu katika kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu bora.
Aidha, amepongeza juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kwa uwekezaji mkubwa unaoendelea kufanyika katika sekta ya elimu kwa lengo la kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji nchini.
“Kaulimbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni “Chakula Bora, Maji Safi Shuleni: Ni Wajibu wa Pamoja,” ambayo inalenga kuhamasisha ushirikiano wa serikali, wadau wa maendeleo na jamii katika kuhakikisha wanafunzi wanapata huduma muhimu shuleni ikiwemo chakula, maji safi na huduma za afya.”amesema Mhe.Ameir
Ameongeza kuwa utekelezaji wa mpango wa chakula na lishe shuleni unahitaji ushirikiano wa sekta mbalimbali, ikiwemo afya, kilimo, maji, maendeleo ya jamii pamoja na wadau wa maendeleo na mashirika yasiyo ya kiserikali.
Pia ameitaka Ofisi ya Rais – TAMISEMI kuendelea kufuatilia vyakula vinavyouzwa katika maeneo ya shule ili kuhakikisha vinakuwa salama kwa matumizi ya wanafunzi na vinaendana na miongozo ya World Health Organization kuhusu afya ya umma.
Katika hatua nyingine, Mhe. Ameir amewataka wadau wa elimu kuendelea kushirikiana na serikali katika kuboresha miundombinu muhimu shuleni ikiwemo ujenzi wa stoo za chakula, mabwalo ya kulia chakula, majiko ya kupikia, matumizi ya nishati safi pamoja na vituo vya kunawia mikono.
“Nawahimiza wazazi kushirikiana na shule kuhakikisha wanafunzi wanapata huduma ya chakula wakiwa shuleni kama ilivyoelekezwa katika Waraka wa Elimu Na. 3 wa Mwaka 2016.”amesema
Hata hivyo amesema ushirikiano wa serikali, wadau na jamii kwa ujumla ni muhimu katika kuhakikisha wanafunzi wanapata lishe bora na mazingira mazuri ya kujifunza, hali itakayosaidia kufikia malengo ya kutoa elimu bora na jumuishi nchini.
Katika maadhimisho hayo, Serikali pia imewashukuru wadau mbalimbali wa maendeleo wakiwemo UNICEF, World Food Programme, GAIN Tanzania na Sanku kwa mchango wao katika kuunga mkono juhudi za kuboresha lishe na huduma ya chakula shuleni.
Akizungumza kwa niaba ya wadau wa Maendeleo ,Naibu Mkurugenzi Mkaazi wa Shirika la chakula Duniani (WFP) Bi.Christin Mendezi,ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa juhudi zake za kuimarisha na kupanua mpango wa utoaji wa chakula mashuleni, wakisema mpango huo una mchango mkubwa katika kuboresha afya, mahudhurio na ufaulu wa wanafunzi.
Kwa mujibu wa takwimu za kimataifa, mpango wa chakula shuleni unaongeza uandikishaji wa wanafunzi kwa asilimia 9 na mahudhurio kwa asilimia 10, huku pia ukisaidia kupunguza tatizo la upungufu wa damu kwa asilimia 20 miongoni mwa watoto wa umri wa kwenda shule.
“Tunaipongeza Tanzania kwa kuendelea kuonesha uongozi katika utekelezaji wa mpango wa chakula shuleni kupitia miongozo ya kitaifa ya lishe shuleni, ushiriki wa jamii pamoja na kuunganisha uzalishaji wa chakula kutoka kwa wakulima wa ndani.”amesema
Naye Mratibu wa Chakula na Lishe kutoka mkoa wa Njombe, Fadhili Msiru, ameeleza namna ambavyo mkoa huo umefanikiwa katika utekelezaji wa mpango wa utoaji wa chakula mashuleni, akibainisha kuwa ushirikiano kati ya jamii, wazazi na Serikali umekuwa chachu ya mafanikio hayo.
Amesema kupitia mpango huo, mahudhurio ya wanafunzi shuleni yameongezeka pamoja na kuboresha hali ya afya na uwezo wao wa kujifunza.








