Home Kitaifa DKT. MWIGULU AWEKA JIWE LA MSINGI SHULE MPYA YA SEKONDARI MBATAKERO

DKT. MWIGULU AWEKA JIWE LA MSINGI SHULE MPYA YA SEKONDARI MBATAKERO

Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba ameweka jiwe la msingi la uzinduzi wa Shule ya Sekondari ya Mbatakero iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro, ambayo imejengwa kupitia mradi wa SEQUIP.

Ujenzi wa shule hiyo ambao umegharimu shilingi milioni 584 utasaidia kuondoa adha wanayopata wanafunzi wa eneo hilo ya kutembea umbali mrefu kwenda shule jirani za sekondari za Roo na Longoi, ambazo ziko umbali wa kilometa 9 kila moja kutoka Kijiji cha Mbatakero, na pia utasaidia kupunguza msongamano wa wanafunzi katika shule hizo.

Akizungumza baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa shule hiyo, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu amesema kuwa ujenzi wa shule hiyo ni matokeo ya maamuzi ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha anaondoa changamoto kwa wananchi.

Kama mlivyosikia, Rais Dkt. Samia anapoelezewa kuna shida, anasema viongozi watatue changamoto hiyo; ndicho kilichotokea katika shule hii ambayo wanafunzi walilazimika kutembea umbali mrefu. Katika kipindi cha miaka minne amejenga zaidi ya shule 1,300 za sekondari na amemaliza kabisa suala lililokuwa linaitwa chaguo la pili (Second Selection).

Katika hatua nyingine, Dkt. Mwigulu amempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai, Dionis Myinga, Mwenyekiti wa Halmashauri Edmund Rutaraka, Mhandisi wa Halmashauri pamoja na Afisa Elimu Sekondari kwa usimamizi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari Mbatakero na kubakiza kiasi cha shilingi milioni 4 ambacho kimetumika kununua samani za ofisi za shule hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!