Home Kitaifa WATEJA 11940 KUUNGANISHWA NA UMEME MKOANI MARA 

WATEJA 11940 KUUNGANISHWA NA UMEME MKOANI MARA 

Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Mtambi amezitaka Kamati za Ulinzi na Usalama pamoja na Wananchi kuhakikisha wanalinda miundombinu ya umeme pamoja na vifaa vitakavyatumikakutekeleza mradi wa Kupelekea Umeme katika Vitongoji 371 mkoani humo.

Mkuu huyo wa Mkoa ametoa maelekezo hayo leo Februari 12, 2026 Ofisini kwake wakati wa kikao na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kilicholenga kumtambulisha rasmi Mkandarasi wa Mradi huo, NAMIS Corporate L.t.d atakaye hudumia Vitongoji 371 vya Mkoani humo.

“Miradi hii inatekelezwa kwa fedha nyingi kwa lengo la kuboresha maisha ya wananchi na asitokee mtu yoyote akafanya ubadilifu wa kuharibu miundombinu ya umeme pamoja na wizi wa vifaa vya utekelezaji wa mradi huu na kukwamisha kutekelezwa kwa mradi huu.

Nitoe onyo kwa mtu yoyote aliyepanga kufanya uharibifu asijaribu katika Mkoa wa Mara hakika tutawakamata, na tukiwakamata tutawachukulia hatua kali za kisheria,” amesisitiza Kanali Mtambi.

Sambamba na hilo amemtaka Mkandarasi anayetekeleza mradi kuhakikisha anautekeleza mradi huo ndani ya muda wa miaka mitatu kama ulivyopangwa kwenye mkataba, na pia alimsisitiza kuzingatia ubora

Kwa upande wake, Mhandis Ernest Makale Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) amesema kwa Mkoa wa Mara Jumla ya Shilingi Bilioni 38.2 itatumika kusambaza umeme katika Vitongoji 371 huku akiwasisitiza kutumia umeme kujikwamua kiuchumi.

“Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ikiwa na lengo la kuendelea kuboresha maisha ya wananchi vijijini. Lengo kuu likiwa Vitongoje vyote ifikapo 2030 viwe na huduma ya umeme

Tuendelee kutoa rai kwa wananchi kuanza kufanya maandalizi ya kupokea mradi huu kwa kuanza kufanya wiring kwenye nyumba zao pamoja na kutumia uwepo wa umeme kujikwamua kiuchumi kwa kufungua miradi mbalimbali vijijini,” amesema Mhandisi Makale.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!