Home Kitaifa SERIKALI YAENDELEA KUFUNGUA FURSA ZA AJIRA KWA VIJANA

SERIKALI YAENDELEA KUFUNGUA FURSA ZA AJIRA KWA VIJANA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu akiwa ameshiriki katika Mkutano wa Mawaziri wa Kazi Duniani (Global Labour Market Conference) unaofanyika Jijini Riyadh, Saudi Arabia tarehe 26 Januari, 2026.

Na: OWM (KAM) – Riyadh, Saudi Arabia

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano Mhe. Deus Clement Sangu amesema Serikali imeendelea kuchukua hatua madhubuti za kuongeza fursa za ajira kwa vijana nchini ikiwemo kushirikiana na sekta binafsi pamoja na wadau wa maendeleo.

Aidha, Mhe. Sangu amesema ushirikiano huo umewezesha wadau wa Maendeleo na sekta binafsi kutoa nafasi mbalimbali za ajira kwa vijana wa Tanzania nje ya nchi, kutokana na uwezo na ujuzi walionao.

Amesema hayo wakati aliposhiriki katika Mkutano wa Mawaziri wa Kazi Duniani (Global Labour Market Conference) unaofanyika Jijini Riyadh, Saudi Arabia Januari 26, 2026.

Amesema, Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imefungua vyuo vya ufundi stadi, ambavyo vinatoa mafunzo ya ujuzi kulingana na mahitaji ya soko la ajira. Ameongeza kuwa, Vyuo hivyo vimekuwa chachu ya kuwawezesha vijana kupata ujuzi wa vitendo, kukuza ubunifu kuongeza ajira.

Vilevile, Waziri Sangu ameseema Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano imeendelea kutekeleza Programu ya Taifa ya Ukuzaji Ujuzi ambapo kupitia Programu hiyo vijana wamekuwa wakipatiwa mafunzo kwa njia ya Uanagenzi yanayolenga kuwajengea uwezo wa kushiriki kikamilifu katika shughuli za uzalishaji, kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira, kuongeza kipato cha mtu binafsi na kuchangia katika ukuaji wa uchumi wa Taifa.

Kadhalika, Mhe. Sangu ameshukuru viongozi wa nchi mbalimbali kwa kuendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania kwa kuongeza fursa zaidi za ajira kwa Watanzania.

Mkutano huo unawakutanisha Mawaziri wa Kazi kutoka nchi zaidi ya 45 duniani na wameweza kujadili na kuweka mikakati ya kushirikiana katika soko la ajira, kuongeza kazi za staha kwa Vijana kwa kuzingatia mchango wa sayansi na teknolojia.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu akiwa ameshiriki katika Mkutano wa Mawaziri wa Kazi Duniani (Global Labour Market Conference) unaofanyika Jijini Riyadh, Saudi Arabia tarehe 26 Januari, 2026.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano Mhe. Deus Clement Sangu akifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Mawaziri wa Kazi Duniani (Global Labour Market Conference) unaofanyika Jijini Riyadh, Saudi Arabia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!