Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda (Mb) amekipongeza Chuo cha Maji baada ya kupokea maelezo ya huduma mbalimbali zinazotolewa na Chuo cha Maji na kujionea Mfumo uliobuniwa na Mwanafunzi wa Chuo hicho
Profesa Mkenda amesema mfumo huo utaleta mafanikio makubwa katika kusaidia Mamlaka za Maji nchini kuendesha shughuli zake kidigitali ikiwemo kudhibiti mivujo, kudhibiti ujazo wa maji kwenye matenki, kudhibiti ubora wa maji, kudhibiti wateja na miundombinu nk. Ametoa salamu hizo za pongezi alipotembelea banda la Chuo kwenye sherehe za kufunga maonesho ya NACTVET yanayotamatishwa leo kwenye Viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma.