Na Neema Kandoro, Mwanza
BAADHI ya wawekezaji wazawa Jijini Mwanza wamepongeza serikali ya awamu ya sita kwa kuweka mazingira rafiki ambayo yamewafanya kumudu kuanzisha miradi ya uzalishaji mali na hivyo kuwezesha upatikananji wa ajira kwa watu katika maeneo yao.
Wakizungumza Jana jijini hapa walisema kuwa kushushwa kwa mtaji wa uwekezaji kutoka dola 100,000 hadi kiwango cha dola 50,000 kuwa ni mojawapo ya motisha ambayo iliwavutia na kuwafanya wawekeze.
Waliongeza kusema kuwa kupatiwa misamaha ya kuingiza mashine toka nchi za nje kuwa nayo ni mojawapo ya ahueni waliyoipata na kufanya baadhi ya vijana kuchangamkia fursa hiyo.
Mmoja wa mwawekezaji kijana mwenye kiwanda cha kutengeneza Cello tepas tepu kiitwacho Joasamwe Investment Kapocha Makongoro alipongeza kuwepo kwa mazingira wezeshi ambayo yamemfanya kupata udhubutu wa kuanzisha mradi huo.
“Kupatiwa muda kuanza kulipa kodi baada kumaliza kujenga kiwanda changu ni faraja kubwa ambayo nimepata” alisema Makongoro.
Aliwataka vijana wenzake kujitokeza katika uwekezaji kwani ni fursa kwa wakati huu ambapo dunia iko kwenye utandawazi.
Makongoro aliongeza kusema kuwa baada kuhitimu masomo yake aliona kuwa kwa vile kuna tatizo la ajira linakumba maeneo yote duniani ameanzisha kiwanda hicho kwa sababu ujasiriamali ni uthubutu.








