Home Kitaifa MABALOZI WATEULE WAIPONGEZA WIZARA KWA MAGEUZI YA ELIMU, WAAHIDI KUSUKUMA AJENDA YA...

MABALOZI WATEULE WAIPONGEZA WIZARA KWA MAGEUZI YA ELIMU, WAAHIDI KUSUKUMA AJENDA YA UMATAIFAISHI

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof Adolf Mkenda leo Aprili 14, 2026 jijini Dodoma amekutana na kufanya mazungumzo na Mabalozi wateule watakaoiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali walizopangiwa.

Katika kikao hicho wamekubalina kuwa elimu, sayansi na teknolojia zitakuwa moja ya agenda za kufanyia kazi ikiwemo suala la umataifishaji elimu.

Mabalozi wateule wameipongeza Wizara kwa mageuzi makubwa ya elimu yanayoendelea kutekelezwa na kuahidi kuichukua agenda ya elimu kuwa ya kimkakati kwa maendeleo ya taifa.

Mabalozi hao ni watakaoiwakilisha Tanzania Saudi Arabia, Zambia, Muscat Comoros, Korea Kusini, Sweden na Umoja wa Mataifa, New York wakiongozwa na Mhe. Balozi Mhandisi Zena Said

Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Naibu Waziri wa wizara hiyo, Katibu Mkuu, Manaibu Katibu Wakuu na baadhi ya Wakurugenzi na Wakuu wa Vitengo wa Wizara hiyo.

¨C11C ¨C12C ¨C13C

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!