Waumini chini wameaswa kutumia Imani ya dini zao kuimarisha misingi ya upendo na amani katika taifa ili kuwezesha wananchi katika maeneo yao kushiriki vizuri katika shughuli za maendeleo Ili kujiletea maendeleo.
Wito huo umetolewa leo jijini Mwanza katika kilele cha sherehe za miaka 52 ya Jumuiya Kuu ya wabaptist TWAUMINIanzania kwenye Kanisa la Nyamanoro ambapo sherehe hiyo ilienda pamoja na mkutano mkuu kwa kanisa hilo hapa nchini.
Alisema sherehe hiyo imefanyika kwa dhamira ya kukumbushana imani ya kanisa hilo pamoja na kuangalia mwelekeo wa kuenenda katika kipindi hiki ambacho kumekuwa na matukio mengi ambayo yanachafua na kufedhehesha baadhi ya makanisa hapa duniani.
Katibu Mkuu wa Baptist Tanzania Mchungaji Elias Kashambagani alisema sherehe hiyo ambayo imewakutanisha washiriki zaidi 1200 toka maeneo tofauti hapa nchini imeazimia watumishi wa makanisa hayo kutumia mahubiri yao kuimarisha misingi ya neno la bwana kama ambavyo imeandikwa kwenye Biblia Takatifu.
“Kuwa na umoja wa wakiristo ambao wanafuata misingi ya Yesu Kristo ndiyo njia pekee ya kuwezesha Kanisa la Mungu kuwatumikia watu na kuunganisha waumini” alisema Mchungaji Kashambagani.
Mchungaji wa Kanisa la Baptist Nyamanoro Peter Mabawa alisema kufikisha kwa kanisa hilo miaka 52 ni ishara njema wa namna ambavyo wamevuka mabonde na milima hivyo kuwaimarisha waumini na kuwa na upendo mkubwa miongoni mwao.
Aliwataka watanzani kuombea amani ya nchi na kutaka waumini kuiunga mkono serikali yao katika jitihada zake za kuliletea taifa maendeleo hivyo wajieupushe na mawazo ya kuwavunja moyo viongozi wa awamu ya sita kwenye dhamira yake ya kufanya kazi na serikali ya Dubhai kwenye bandari ya Daressalaam.
Naye Katibu wa Kanisa la Baptist Tanzania Nyamanoro Vicent Tebho alisema tukio hilo limeenda sambamba na watumishi wa neno la Mungu kufundishana maarifa ya kukua kiroho Ili wakatowe injili ya mafanikio kwa watu.
Alisema dhamira ya serikali kuruhusu kila muumini kuabudu dhehebu analolitaka ni hatua nzuri katika kujenga taifa lenye usawa linalozingatia matakwa ya watu wote bila ubaguzi wowote








