Home Kitaifa WATU 21 WAFARIKI KATIKA MAFURIKO MOROCCO

WATU 21 WAFARIKI KATIKA MAFURIKO MOROCCO

Na: Secilia Edwin

Watu 21 wamefariki dunia na wengine 32 kujeruhiwa baada ya mvua kubwa kunyesha na kusababisha mafuriko yaliyotokea jana Jumapili katika jimbo la pwani ya Atlantiki la Safi, lililopo kilomita 330 (maili 205) kusini mwa Rabat.

Kwa mujibu wa taarifa za mamlaka za Morocco zilizotolewa usiku wa kuamkia leo, Desemba 15, 2025, wengi wa waliojeruhiwa wamesharejea nyumbani.

Mvua hiyo iliyonyesha kwa saa moja ilisababisha uharibifu wa miundombinu, nyumba na maduka, huku baadhi ya barabara zikikatika na juhudi za uokoaji zikiendelea. Morocco kwa sasa inakabiliwa na mvua kubwa na theluji katika milima ya Atlas, hali inayojitokeza baada ya miaka saba ya ukame uliosababisha baadhi ya mabwawa kupungua kwa kiasi kikubwa.

Hali hiyo imeleta changamoto kwa wananchi wa Safi, huku mamlaka zikiwahakikishia usalama na msaada kwa walioathirika.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!