Home Kitaifa WANANCHI UVINZA WAFUNGUKA UPATIKANAJI HUDUMA ZA AFYA

WANANCHI UVINZA WAFUNGUKA UPATIKANAJI HUDUMA ZA AFYA

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

WANACHI wa wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma wamesema kuwa maboresho makubwa yaliyofanywa kwenye sekta ya afya wilayani humo ikiwemo ujenzi wa hospitali ya wilaya hiyo umewezesha kusogezwa huduma za afya karibu na wananchi lakini pia kupunguza gharama kwa wananchi hao kufuata huduma za matibabu.

Wananchi hao wametoa kauli hiyo kwa waandishi wa Habari waliokuwa wakifanya ziara kutembelea miradi ya afya na elimu katika wilaya hiyo ambapo wamesema kuwa maboresho hayo yamekuwa na faida kubwa katika Maisha ya kawaida ya wananchi hao.

Akitoa ushuhuda wa mafanikio katika maboresho hayo mmoja wa wananchi wa wilaya hiyo, Hamisi Fataki ambaye alilazwa na kufanyiwa upasuaji katika hospitali ya wilaya Uvinza alisema kuwa kabla ya huduma hiyo hakuwa na wazo la kutibiwa na kupata huduma za upasuaji katika hospitali ya wilaya Uvinza akili yake ikiwa Kwenda Bugando Mwanza au Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Kwa upande wake Mwana Mama Liberata Gabinus Mkazi wa kijiji cha Mwamila wilaya ya Uvinza alisema kuwa hospitali hiyo imeondoa usumbufu wa kutembea umbali mrefu lakini kupunguza katika kufuata huduma za matibabu

Akielezea kuhusu ujenzi wa hospitali hiyo ya wilaya Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Zuwena Masudi alisema kuwa serikali imetoa kiasi cha shilingi Bilioni 3.4 tangu mwaka 2021 ujenzi ulipoanza na kwamba kwa sasa huduma zote muhimu za matibabu ikiwemo upasuaji zinafanyika kwenye hospitali hiyo ya wilaya zikiwemo huduma ambazo hazikuwa zikifanyika mahali popote wilayni humo.

Mganga huyo Mfawidhi wa hospitali ya wilaya Uvinza alisema kuwa kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa hospitali hiyo kumetoa unafuu mkubwa kwa wananchi katika kupata huduma za matibabu ukilinganisha na kabla ya ujenzi huo ambapo wananchi wengi walikuwa wakitegemea kupata huduma kutoka hospitali ya rufaa ya mkoa Kigoma Maweni Kilometa Zaidi ya 80 kutoka hapo

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!