Home Kitaifa WANANCHI KIJIJI CHA NYASAUNGU KUANZA KUPATA HUDUMA ZA AFYA KWENYE ZAHANATI DISEMBA...

WANANCHI KIJIJI CHA NYASAUNGU KUANZA KUPATA HUDUMA ZA AFYA KWENYE ZAHANATI DISEMBA 2024

Na Shomari Binda-Musoma

WANANCHI wa Kijiji cha Nyasaungu chenye vitongoji 5 kilichopo jimbo la Musoma vijijini wataanza kupata huduma za afya kwenye zahanati yao ifikapo mwezi disemba.

Kijiji hiki ni moja ya vijiji vitatu vya Kata ya Ifulifu huku vijiji vingine ni Kabegi na Kiemba ambavyo kila kimoja kina zahanati yake.

Ujenzi wa zahanati hiyo ulianza kwa kutumia michango ya fedha kutoka kwa wanakijiji na mbunge wa jimbo la Musoma Vijijini Profesa Sospeter Muhongo.

Mbunge huyo aliendesha harambee mbili za kupata fedha za kuanza ujenzi wa zahanati hiyo ambazo zilikuwa na mafanikio makubwa.

Licha ya harambe hizo za mbunge wanakijiji wanachangia nguvukazi kwenye ujenzi wa zahanati yao.

Hadi sasa serikali kuu imeshatoa kiasi cha milioni 100 kwaajili ya kuendelea na ujenzi huo

Jengo kuu la zahanati linakamilishwa,
choo chenye matundu matatu kinajengwa huku
mkandarasi akipewa mkataba wa kukamilisha ujenzi wa zahanati hiyo upande jengo kuu na choo unaoishia tarehe 30 Novemba 2024.

Kujitolea kwa wanakijiji wa Nyasaungu kunaharakisha maendeleo ya kijiji kwa huduma muhimu zikiwemo za afya,elimu na kijamii.

Wanakijiji wa Nyasaungu na viongozi wao wa ngazi zote wanaishukuru sana serikali chini ya uongozi mzuri wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kutoa fedha za kuchangia miradi ya maendeleo ya Kijiji cha Nyasaungu cha jimbo la Musoma Vijijini

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!