Wafanyakazi zaidi ya 70 wanaofagia barabara mbalimbali za jiji la Mwanza wamelalamikia malimbikizo ya mishahara yao ya miezi sita na kuomba serikali kuingilia kati ili kuwanusuru na ugumu wa Maisha wanaokutana nao kwa kushindwa kulipa kodi, kununua chakula pamoja na kununua mahitaji ya wanafunzi.


Baada ya jitihada za kuwatafuta wahusika wa kampuni hiyo kugonga mwamba mkuu wa wilaya ya Nyamagana Amina Makilagi akizungumza kwa njia ya simu akasema alishawahi kuzungumza na viongozi hao na kuwaagiza wawalipe stahiki wafanyakazi hao lakini wamekaidi agizo hilo.









