Home Kitaifa TAKUKURU MARA YATAKA VIFAA VISIVYO NA UBORA KUTOTUMIKA KWENYE MIRADI

TAKUKURU MARA YATAKA VIFAA VISIVYO NA UBORA KUTOTUMIKA KWENYE MIRADI

Na Shomari Binda-Musoma

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Mara limesimama kidete kuhakikisha vifaa visivyokuwa kuwa na ubora kutumika kwenye miradi ya maendeleo.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu mkuu wa taasisi hiyo mkoa wa Mara, Antony Gang’olo wakati akitoa taarifa ya kazi kwa kipindi cha miezi mitatu kuanzia januari hadi machi.

Amesema kwa kuzingatia serikali inapeleka fedha nyingi kwenye miradi ya maendeleo Takukuru mkoa wa Mara imefanya kazi ya kuzuia vifaa visivyo na ubora kutumika

Naibu mkuu huyo wa Takukuru amesema katika kipindi hicho katika sekta ya afya ilifatiliwa miradi mitatu kwenye wilaya za Bunda,Butiama na Serengeti yenye thamani zaidi ya bilioni 1.

Amesema katika ufatiliaji huo ilibainika kuna vifaa vya vya ujenzi vyenye thamani ya shilingi 340,000.00 ambavyo vilinunuliwa zahanati ya Kijiji cha Buruma wilayani Butiama bila uhitaji.

Antony amesema Takukuru ilihakikisha vifaa hivyo vinarudishwa na kiasi hicho cha fedha kinarudishwa kwenye akaunti ya Kijiji.

Amesema katika sekta ya maji pamoja na elimu ufatiliaji pia umefanyika kwenye miradi inayotekelezwa na vifaa vilivyobainika kutokuwa na ubora vilirudishwa.

Aidha katika kipindi hicho Takukuru mkoa wa Mara imefanya ufatiliaji wa mifumo ili kubaini mianya ya Rushwa na kutoa ushauri kwa wahusika kuona namna bora ya kurekebisha mapungufu yaliyobainika.

Amesema katika eneo hilo ilibainika pia wapo wakusanyaji wa mapato kwenye halmashauri ambao sio watumishi na wengine hawapeleki fedha benki baada ya kukusanya.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!