
Serikali imeahidi kuendelea kuhamasisha wawekezaji kuwekeza nchini, kwa kuweka mazingira wezeshi ikiwemo miundombinu na kutoa msaada katika kutatua changamoto mbalimbali zitakazojitokeza ili kuongeza ajira, Pato la Taifa na kuchochea ukuaji wa uchumi wa viwanda shindani.

Hayo yamesemwa Desemba 11, 2025 na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe Judith Kapinga (Mb) akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Bi Khadija Nasri Ali, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Viwanda Bw. Juma Mwambapa, Katubu Tawala MsaidiI sehemu ya Uwekezaji Viwanda na Biashara Mkoa wa Pwani pamoja na Wawakilishi wa Taasisi za TBS, FCC, BRELA, TANTRADE, TIRDO na TISEZA wakati akitembelea Kiwanda cha Goodwill na KEDA Viwanda vya Good
alipofanya ziara ya kutembelea viwanda vya Goodwill Ceramic na Keda Ceramics vilivyopo wilayani Mkuranga, Mkoa wa Pwani.

Aidha, Waziri Kapinga alibainisha kuwa lengo la ziara hiyo nikujionea shughuli za Uzalishaji, kusikiliza na kutatua changamoto zilizopo katika Viwandani hivyo vinyasa bidhaa kwa kutumia malighafi za ndani na kuzalisha bidhaa zenye ubora zinazotumia Nembo ya Made in Tanzania katika kuuza bidhaa hizo katika Masoko ya Kimataifa ikiwemo Soko la Marekani na Italia.

Pia, aliwapongeza viongozi wa viwanda hivyo kwa kutoa ajira nyingi kwa vijana ambapo Kiiwanda cha Goodwil kinachangiza ajira za moja kwa moja 1,600, huku upande wa kiwanda cha KEDA kikitoa ajira za moja kwa moja 5,000 na zisizo za moja kwa moja 40,000 ikiwa ni moja wapo ya jitihada za kutimiza ahadi ya kufikia ajira milioni nane.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Khadija Nasri Ali, alisema wataendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji kuja kuwekeza nchini hususani Wilaya y Mkuranga ambayo huku akisisitiza kuwa nchi ipo salama na inahitaji wawekezaji kuja kwa wingi.

Naye, Mkurugenzi wa Msimamizi wa Kiwanda cha Goodwill, Bw. Eric Jiang na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha KEDA Bw. Wayne Zhong, wameishukuru Serikali kwa ushirikiano mzuri wanaoutoa kwa wawekezaji ambao umekuwa chachu kwa wao kuja kwa wingi kuwekeza na kufanya Biashara nchini kwa kuwa Tanzania ni nchi salama inayofaa kwa wawekezaji kuja kuwekeza.
Wakizungumza kwa niaba ya wafanyakazi, Bw.John Chimwejo kutoka KEDA na Bw. Jelly Marandu kutoka Goodwill wameziomba Taasisi za umma na binafsi kuendelea kutoa ushirikiano kwa viwanda hivyo kwa kuwa vinasaidia kuongeza ajira kwa Vijana na kukuza uchumi kwa jamii na Taifa kwa ujumla.








