Home Kitaifa RC MTANDA ATOA HAMASA YA MILIONI 2 KWA WACHEZAJI BIASHARA UNITED WAKIIFUNGA...

RC MTANDA ATOA HAMASA YA MILIONI 2 KWA WACHEZAJI BIASHARA UNITED WAKIIFUNGA MBUNI FC 2-0

-AWAITA WANACHAMA NA WADAU KUONGEZA HAMASA

Na Shomari Binda-Musoma

MKUU wa mkoa wa Mara Said Mtanda ameahidi kutoa kiasi cha shilingi milioni 2 kama hamasa kwa wachezaji kufuatia ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mbuni fc.

Ushindi huo ni wa kwanza kwa timu hiyo kwenye mzunguko wa pili wa Championship na kushika nafasi ya pili kwa kufikisha pounti 32.

Akizungumza kwenye dimba la Karume mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo amesema hamasa zaidi inahitajika ili timu hiyo iweze kurejea ligi kuu msimu ujao.

Amesema kwa upande wake anaendelea na hamasa alizojiandaa nazo kwa wachezaji na benchi la ufundi na upande wa wanachama na wadau wanayo nafasi ya kufanya jambo kila mchezo ili kuongeza hamasa

Mkuu huyo wa mkoa amesema zipo hamasa za kununua magoli,pasi ya mwisho ya goli na hamasa nyingine ambazo zinaweza kuongeza chachu ya ushindi.

Niwapongeze wachezaji na benchi la ufundi kwa ushindi wa leo dhidi ya Mbuni fc na kwa ushindi huo vijana watapata hamasa ya milioni 2.

Wanachama na wadau wengine wa soka mkoa wa Mara wanayo nafasi ya kujitokeza kuongeza hamasa kwenye mzunguko huu wa pili kwenye kila mchezo ili tuweze kurejea ligi kuu”,amesema Mtanda.

Amesema licha ya motisha kwa wachezaji na benchi la ufundi ameahidi kulipia miezi 6 eneo la kambi ya timu hiyo pamoja na baadhi ya matumizi ya kambi.

Golikipa wa timu hiyo Devid Kisu amesema hawatamuangusha mkuu wa mkoa na wstapambana kuhakikisha malengo ya kurejea ligi kuu msimu ujao yanafanikiwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!