Home Kitaifa RC MTAMBI APOKEA UANZISHWAJI WA TUZO ZA WAANDSHI WA HABARI MKOA WA...

RC MTAMBI APOKEA UANZISHWAJI WA TUZO ZA WAANDSHI WA HABARI MKOA WA MARA

Na Shomari Binda-Musoma

MKUU wa mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi amesema amepokea wazo la uanzishwa wa tuzo kwa Waandishi wa Habari mkoa wa Mara.

Wazo hilo limetolewa na klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Mara ( MRPC) kwenye mdahalo uliofanyika jana julai 5 mjini hapa uliokuwa ukijadili fursa za uwekezaji mkoa wa Mara na sehemu bora ya kuishi

Tuzo hizo zitakazoanza kutolewa desemba mwaka huu zitahusu Waandishi watakaoandika habari za kutangaza sekta mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwavutia wawekezaji mkoani Mara.

Akizungumza kwenye mdahalo huo mkuu wa mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi amesema wazo hilo ni zuri na litaongeza chachu kwa Waandishi wa Habari kuzitangaza fursa zilizopo.

Amesema mkoa wa Mara unazo fursa nyingi ikiwemo hifadhi bora ya Serengeti, ziwa victoria,mifugo na nyingine nyingi ambazo zikitangazwa vizuri zitauinua mkoa.

Rc Mtambi amepongeza mdahalo huo ulioandaliwa na klabu ya Waandishi wa Habsri mkoa wa Mara uliolenga kutangaza fursa zilizopo mkoa wa Mara na sehemu bora ya kuishi.

” Niwapongeze sana kwa mdahalo huu mliouandaa na kualika wadau mbalimbali kuzungumzia fursa zilizopo kwenye mkoa wetu.

” Baada ya hapa tunaweza kukutana baada hata ya miezi 4 kuangalia yale yaliyojadiliwa na namna yanavyokwenda na nipongeze hili lililofanyika”,amesema.

Mwenyekiti wa klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Mara Mugini Jacob amemshukuru mkuu huyo wa mkoa kwa kukubali kushiriki mdahalo huo na kupokea wazo la uanzishwaji wa tuzo.

Amesema Waandishi wa Habari mkoa wa Mara wapo tayari kushirikiana na ofisi ya mkoa wa Mara katika kutangaza fursa zilizopo.

Akizungumzia tuzo hizo Mugini amesema zitaendana na fedha kwa watakaofanya vizuri kuandika na kutangaza mambo mazuri ya mkoa wa Mara.

Kwenye mdahalo huo wazungumzaji mbalimbali wamezungumza na kutoa mawazo yatakayowavutia wawekezaji ili kuja kuwekeza mkoa wa Mara.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!